Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamemuomba rais wa Marekani Donald Trump kulinda usalama wao katika mkutano wake wa kilele na Rais wa Urusi Vladimir Putin unaotarajiwa kufanyika baadae wiki hii kujadili vita vya Ukraine.
Viongozi hao wanataka kuwa na ushawishi katika mkutano huo utakaofanyika siku ya Ijumaa ila hawakualikwa kuhudhuria.- Haijawa wazi pia iwapo Ukraine yenyewe itahudhuria mkutano huo wa Alaska.
Awali, Trump alisema anataka kukutana na Putin kuona iwapo ana nia ya kweli ya kuvimaliza vita hivyo ambvayo vipo katika mwaka wake wa nne.
“Marekani Yapanga Mkutano wa Trump, Putin na Zelensky: Suluhu ya Vita ya Ukraine Yazidi Kuwa Karibu”
Trump aliwashitua washirika wake wa Ulaya aliposema kwamba Ukraine ni lazima iyaachie maeneo yake kwa Urusi na Urusi pia ni lazima ikubali kubadilishana maeneo.
