Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewahimiza wananchi kuendeleza utaratibu wa kuiombea nchi amani ili kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo unafanikiwa kwa ufanisi.

Akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ijumaa, Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi leo tarehe 7 Novemba 2025.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu kwa amani, ni muhimu kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuendelea kumuomba ili amani hiyo idumu.

Halikadhalika, Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kazi nzuri iliyofanyika kuombea amani wakati wa uchaguzi inapaswa kuendelezwa kwa juhudi kubwa zaidi.

Rais Mwinyi amesisitiza kuwa ni neema kubwa kwa Zanzibar kubaki na umoja, amani, utulivu, na mshikamano baada ya uchaguzi, na kuwataka viongozi wa dini na waumini kuendelea kuiombea nchi ili ibaki salama na yenye maendeleo.