Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza Kikao cha Kwanza cha Baraza la Mapinduzi (BLM) cha Kipindi cha Pili cha Serikali ya Awamu ya Nane.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 29 Disemba 2025, Ikulu, Zanzibar.
Kikao hicho cha BLM pia kimeambatana na uapisho, ambapo Rais Dkt. Mwinyi amemuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe. Mgeni Khatibu Yahya, aliyemteua hivi karibuni.
Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Mgeni alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Pemba.





