Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa uteuzi wa Mawaziri wateule unalenga kuimarisha kasi ya maendeleo katika kipindi cha pili cha Awamu ya Nane.
Rais Dkt. Mwinyi amesema kwamba kwasasa kutakua na jumla ya Wizara 20 badala ya 18 zilizokuwepo katika kipindi cha kwanza, ikiwa ni hatua ya kuongeza ufanisi katika kusimamia sekta mbalimbali Serikalini.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 13 Novemba 2025, Ikulu Zanzibar, katika hafla ya kuwatangaza Mawaziri wateule. Hafla hiyo imehudhuliwa na Waandishi wa Habari na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Akitangaza Mawaziri na Naibu Mawaziri hao wateule, Dkt. Mwinyi ameyataja majina yao pamoja na Wizara watakazoongoza kama ifuatavyo:
MAWAZIRI
- DKT. HAROUN ALI SULEIMAN, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora
- MHE. DKT. SAADA MKUYA SALUM, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu
- MHE. DKT. JUMA MALIK AKIL, Waziri wa Fedha na Mipango
- MHE. IDRISSA KITWANA MUSTAFA, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ
- MHE. SHARIFF ALI SHARIFF, Waziri wa Kazi na Uwekezaji
- MHE. HAMZA HASSAN JUMA, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi
- MHE. RAHMA KASSIM ALI, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi
- MHE. LELA MUHAMED MUSSA, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali
- MHE. SHAABAN ALI OTHMAN, Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji
- MHE. SULEIMAN MASOUD MAKAME, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo
- MHE. NADIR ABDULLATIF ALWARDY, Waziri wa Maji, Nishati na Madini
- MHE. MASOUD ALI MOHAMED, Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi
- MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
- MHE. ANNA ATHANAS PAUL, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
- MHE. MUDRIK RAMADHAN SORAGA, Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu
- MHE. RIZIKI PEMBE JUMA, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
NAIBU MAWAZIRI
- MHE. BADRIA ATAI MASOUD, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
- MHE. DKT. HAMAD OMAR BAKARI, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
- MHE. ALI ABDULGULLAM HUSSEIN, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo
- MHE. ZAWADI AMOUR NASSOR, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
- MHE. SALHA MOHAMED MWINJUMA, Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi
- MHE. SEIF KOMBO PANDU, Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini
- MHE.DKT.SALUM SOUD HAMID, Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo
- MHE. MBOJA RAMADHAN MSHENGA, Naibu Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi
- MHE. MOHAMED SIJAMINI MOHAMED, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu
- MHE. HASSAN KHAMIS HAFIDH, Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji
- MHE. KHADIJA SALUM ALI, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali
Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa nafasi za Wizara nne ameziacha wazi kwa muda, hadi Serikali ikamilishe makubaliano na Chama cha ACT Wazalendo kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Wizara zilizoachwa wazi:
- Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
- Wizara wa Afya
- Wizara wa Utalii na Mambo ya Kale
- Wizara wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda
Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa uteuzi huo umezingatia uwiano wa kijinsia, uwakilishi wa pande zote mbili za Unguja na Pemba, pamoja na uzoefu wa viongozi katika sekta husika


