Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameahidi kununua boti mbili za doria ndani ya Ziwa Victoria.
Pia ameahidi wananchi kupitisha uzio pembezoni mwa ziwa ili kuzuia mamba ambao wanahatarisha usalama wa watumiaji.
Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza leo Oktoba 7,2025.







