Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa Sh milioni 50 kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Nyalikungu wilayani Maswa Mkoa wa Simiyu.

Akiwasilisha mchango kwa niaba ya Rais Samia, wilayani Maswa, jana, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alisema Dk. Samia anatambua mchango wa viongozi wa dini katika kuimarisha umoja na amani ya nchi.

“Sasa nawapa salamu za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Rais Dk. Samia na kwa sababu nilimwambia nimealikwa mahali hapa kuwa mgeni rasmi kwa ajili ya mchango wa Kanisa na yeye ni mchamungu akaniambia na yeye atachangia Sh milioni 50,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha, aliwaomba viongozi wa kanisa kuendelea kuiombea nchi hususan katika mwaka huu wa uchaguzi mkuu ufanyika kwa uhuru na amani.