Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko katika muundo wa baadhi ya wizara pamoja na uteuzi wa viongozi mbalimbali wa mikoa na makatibu wakuu. Mabadiliko hayo yamelenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya serikali na kuimarisha huduma kwa wananchi.




