
Na Aziza Nangwa JamhuriMedia, Dar es Salaam
Wizara ya Nishati imeagizwa kuimarisha akiba ya nishati ya mafuta ili kuongeza uwezo wa nchi kujilinda dhidi ya misukosuko ya kimataifa.
Kauli hiyo imetolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa matanki ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, eneo la Kigamboni.
Dkt Samia amesema kuwa, mbali na uhifadhi huo, pia itasaidia kujilinda na mabadiliko ya bei katika soko la dunia.
Amesema uwekezaji wa serikali katika ujenzi wa matanki hayo ya kupokea mafuta ni hatua ya kimkakati katika kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha uwekezaji wa kikanda na kimataifa.
‘’Huu ni uthibitisho kwamba kama taifa tumeamua kuilinda kikamilifu jiografia ya nchi yetu, kama lango kuu la kuhudumia nchi zisizo na bahari na zilizounganishwa na milango ya baharini.
Tumedhamiria kuhudumia wenzetu kibiashara, na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara ndani ya ukanda huu,’’ amesema.

Amesema Bandari zetu, ikiwemo hii ya Dar es Salaam, zina mchango mkubwa sana katika kukuza uchumi wa nchi yetu na ustawi wa watu.
‘’Serikali imeendelea kufanya maboresho ya miundo mbinu katika Bandari za Bahari ya Hindi pamoja na maziwa makuu. Bandari kavu pamoja na ushirikishwaji wa sekta binafsi
Bandari kavu pamoja na ushirikishwaji wa sekta binafsi, katika kufikia malengo yetu ya kiuchjumi kama sera zetu zinavyosema kwamba maendeleo yetu hatukwenda peke yetu tumekubaliana kuishirikisha sekta binafsi katika safari yetu ya maendeleo na tija ndiyo hii leo’’amesema.
Amesema maboresho yote yaliyofanyika katika sekta hii ya uchukuzi, yameongeza uwezo wa utoaji huduma na kuleta ushindani kwa kuleta a mageuzi makubwa hasa katika Bandari ya Dar es salaam kwa kuhudumia meli kubwa .
‘’Baada ya maboresho , walijitokeza wawekezajia wengi sana ili waingie kwenye Bandari zetu , mpaka sasa tumeweza kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi ya forodha sh.trion 12 .31 mwaka 2024 /2025 ikilinganishwa na sh.trion 7.3 za mwaka 2020 /2021 ‘’amesema.
Amesema katika mafanikio haya ni muhimu kutambua mchangp wa sekta binafsi, ambao umeongeza ufanisi na kazi ya mageuzi ya bandari kwani ushirikishwaji wao umeleta tija na kuongeza kasi ya mageuzi tulio yakusudia.

‘’Ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari zetu, ulikuwa ni uamuzi wa kimkakakati uliohitaji ujasili na dhamira thabiti kama nilivyosema fedha zile zinapoingia kwenye sekta binafsi kupitia bandari zetu’’amesema
Amesema uboreshaji wa Bandari baada ya kushirikisha sekta binafsi ,umesaidia Mamlaka ya Bandari, kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza ufanisi kwenye biashara.
‘’Zile fedha tuliziacha ndiyo hizo sasa, zinajenga miradi kama mradi huu wa mantaki ya kupokkelea mafuta’’amesema
Amesema kadri bandari inavyokuwa na kuongeza uwezo wa kuongeza shehena, ndiyo inavyo hitaji miundo mbinu inayoendana na mnyororo mzima wa biashara
‘’Leo hii tunasogea hatua nyingine muhimu ya kuanza ujenzi wa matanki ya kupokea mafuta, yenye uwezo wa mita za mlaba 378000 kwa wakati mmoja.

Faida yake ni kuondosha changamoto, kwani kabla ya mradi huu mamlaka ya TPA haikuwa na mataki yake ya kupokea mafuata hivyo kukamilika kwa mradi huu kutaimarisha usalama wa nishati ya mafuata kwa taifa.
Dkt Samia amesema hatua ya uwekeji wa jiwe hilo ,ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi au uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ambapo walitoa ahadi kwa wananchi
‘’Tuna kwenda kuimarisha miundo mbinu ya kisasa ya usafiri na usafirishaji kwani tuliahidi ,kuongeza kasi ya miradi ya kimkakati yenye kuleta matokeo huu ukiwa mmoja wao
Wizara ya Uchukuzi na Mamalaka ya Bandari nawataka muhakikishe, mradi huu unatekelezwa kwa wakati na kwa ubora unao zingatia viwango vya kimaifa kwa uhifadhi wa mazingiara’’amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Plasduce Mbossa amesema ,Serikali ya awamu ya sita kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliingia mkataba na Wakandarasi wabia
Kwa ajili ya mradi wa Usanifu na Ujenzi wa Matanki (Tanks Farm) ya Kupokea na kusambaza Mafuta wenye gharama ya shilingi za Tanzania Bilioni 678.6 ikijumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Mbosa amesema mradi huu umepangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miezi ishirini na nne pamoja na muda wa miezi kumi na miwili (12) wa kipindi cha matazamio.
Ili kuepuka athari ambazo zingeweza kujitokeza katika mnyororo wa upokeaji na usambazaji wa mafuta nchini, mradi huu umepangwa kutekelezwa kwa awamu mbili.
Amesema utekelezaji wa mradi huo, kwa awamu ya kwanza unafanyika katika eneo la viwanja na. 1 hadi 4, kitalu q, Tungi–Kigamboni, Dar es salaam na utakapokamilika, utakuwa na jumla ya matanki kumi na tano (15) yenye uwezo wa kupokea na kusambaza mafuta yenye jumla ya mita za ujazo 378,000.
‘’Miundombinu ya mradi huu itawezesha TPA kupokea aina tatu za mafuta ambazo ni: mafuta ya dizeli kiasi cha mita za ujazo 162,000, mafuta ya petroli kiasi cha mita za ujazo 135,000 na mafuta ya ndege (Jet – A1) kiasi cha mita za ujazo 81,000.
Awamu ya pili ya mradi huu itahusisha ujenzi wa magati ya kuhudumia shehena za mafuta, ambayo yatakuwa na miundombinu ya usafirishaji wa mafuta kutoka kwenye meli kuja moja kwa moja katika matenki haya’’amesema.

Amesema hadi kufikia tarehe 03 Machi, 2026 utekelezaji wa jumla wa mradi ,umefikia asilimia 41 na una tarajiwa kukamilika tarehe tarehe 03 Februari 2027 ambapo kwa sasa kazi zimekamilika kwa asilimia 100 ni Maandalizi ya eneo la ujenzi, ikijumuisha kuondoa udongo ,dhaifu na mchafu wa kiasi cha mita za ujazo elfu 53.3 .
‘’Ujenzi wa uzio (fencing wall) wenye urefu wa mita 1,130 (kati ya mita1,265 za uzio wote wa ukuta , Ujenzi wa majengo ya ofisi za Mkandarasi na Mhandisi Mshauri na d) Ujenzi wa nguzo (piles) 1,087 za matanki; na Ujenzi wa kofia rundo (pile caps) kumi na tano (15)’’amesema.
Hadi kufikia Februari 2026, Serikali imesha mlipa Mkandarasi kiasi cha sh.bilioni 113.6,Mhandisi Mshauri malipo ya awali ya jumla ya Dola za Marekani milioni 1.5 sawa na sh.bilioni 3.5 na hivyo kufanya jumla ya malipo ya mradi huu hadi sasa kuwa shilingi za Tanzania bilioni 117.1’’amesema.
Amedai baada ya kukamilika mradi huo unatarajiwa kuleta manufaa kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za bandari ,kwa kupunguza muda wa kuhudumia meli za mafuta kutoka wastani wa siku 22 za sasa hadi wastani wa siku 7 kwa meli moja;
Kuondoa gharama ya Dola za Marekani 25,000 sawa na sh.milioni 58 kwa siku, ambayo hulipwa kama tozo kutokana na kuchelewa kushusha shehena ya mafuta, na hivyo kuondoa mzigo wa gharama ambao hubebwa na mtumiaji wa mwisho
Amesema utaweza kuboresha ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam kibiashara, kwa kuvutia zaidi meli za kimataifa kutokana na kuongezeka kwa ufanisi wa utoaji huduma.
Amesema utekelezaji wa mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango, kabambe wa maendeleo ya bandari nchini wa miaka 25 kuanzia mwaka 2020 hadi mwaka 2045.
Ambapo mpango huo unalenga kuongeza, uwezo wa miundombinu ya Bandari nchini pamoja na kuongeza ufanisi na tija.




