Rais Samia amesikitishwa sana kusikia taarifa za kifo cha Rais wa zamani wa Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria, Mheshimiwa Muhammadu Buhari.
Kwa mujibu wa tarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Instagram amesema kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ametoa pole za dhati kwa Mheshimiwa Bola Ahmed Tinubu, Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria, familia ya Rais Buhari, na wananchi wote wa Nigeria.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. 🕊️
