Na Mwandishi Wetu

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia Katibu Mkuu wake, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo imeeleza kwamba imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka ikitaarifu kuwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Hamphrey Polepole aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kumuondolea hadhi ya ubalozi. Mwananchi imeripoti.

Uamuzi huo wa Rais ni chini ya mamlaka aliyonayo chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Rais Samia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya utumishi wa umma, amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.

Kwa mujibu wa barua hiyo, uamuzi huo umeanza tangu Julai 16, mwaka 2025.

Balozi huyo alijiuzuru siku ya Jumatatu akidai hawezi kuwa sehemu ya serikali isiyojali misingi ya haki, sheria na katiba ya nchi.