Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa CISM Kanda ya Afrika Meja Jenerali Maikano Abdullahi kutoka Nigeria mara baada ya kupewa Tuzo ya Heshima ya Uanachama wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (Honorary Member), Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Agosti, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kutunukiwa Nishani pamoja na kupewa Tuzo ya Heshima ya Juu ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Agosti, 2025.
Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya kutunukiwa Nishani ya CISM kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salam tarehe 14 Agosti, 2025.