Na Berensi China, JamhuriMedia, Simiyu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Wazazi nchini kuwapa fursa ya kupata elimu vijana ili waweze ujuzi na kujiajri kutokana na serikali kuwekeza kwa kujenga Shule za Msingi, Sekondari na Amali.
Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akiwa jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali Mwamapalala iliyoko wilayani Itilima Mkoani Simiyu kwa niaba ya Shule 26 zinazojengwa nchini.
Rais Samia amesema kuwa serikali umeamua kubadili mwelekeo ili Mwanafunzi anapomaliza kidato Cha nne aweze kujiajiri na kiajiriwa ambapo serikali imedhamiria kujenga Shule za Amali na shule.za Ufundi
“Shule za Amali ni Shule zinazompa Mwanafunzi ujuzi wa kiajiriwa au kijiajiri na tunazijenga nyingi…nimeweka jiwe la Msingi hapa Itilima kwa niaba ya Shule zote zinazoendelea na ujenzi nchi mzima na nikienda kufungua moja,.nitafungua kwa niaba ya shule zote” amesema”
Alimshukuru Mkandarasi anayetekeleza Mradi huo huku akimataka kuharakisha ukamilishaji ili kufikia mwezi January 2026 wanafunzi waweze kuanza masomo rasmi.

Alisema Shule hiyo itaanza na wanafunzi 300 ambao serikali imejipanga kuwajengea uwezo na kuwapa ujuzi sababu uwezo wa serikali kuwaajiri haupo na kupitia ujuzi huo wataajiriwa katika sekta binafsi.
Alifafanua kuwa ujenzi wa Shule hizo za Amali na Ufundi ni uwekezaji ambao serikali imeufanya Kwa kujenga Shule hizo nyingi na kwamba tangu mwaka 2022 jumla ya Shule za Msingi 42 zimejengwa na kuongeza idadi kutoka 564 hadi 606 katika Mkoa wa Simiyu.
“Jumla ya Shule 31 za Sekondari zimejengwa na kuongeza idadi kutoa 152 hadi 183 ambazo zimeongeza fursa kwa vijana wetu… serikali tunatumia fedha nyingi kujenga Shule za Msingi, Sekondari za Ufundi na tumeanza kuleta Matawi ya vyuo vikuu, tafadhali wapeni vijana fursa ya kutumia pesa za.elimu ili wajijenge Kwa maisha yao ya leo.na baadae” amesema.
Aliongeza kuwa shule hiyo bado iko kwenye ujenzi lakini bado inahitaji vifaa vya mabweni, vifaa vya kujifunza ni kufundishai ambapo baada ya kukamilika ambapo Waziri wa TAMISEMI na Waziri wa Elimu kuahidi kuleta vifaa hivyo.
Aliongeza kuwa wataongeza Walimu zaidi licha ya kuwepj Walimu 5 ili kuhakikisha utoaji wa Elimu inakidhi Malengo na mahitaji ya serikali.
Kwa upande wake waziri wa elimu profesa Adorf Mkenda amesema kujengwa kwa shuke za amali hapa nchini kutasaidia vijana wengi kujiajili pindi wamalizapo elimu ya sekondar huku mbunge wa jimbo la itilima Njalu silanga akiipongeza serikali kwa ujenzi huo.
Ikiwa Leo ni siku ya tatu ya ziara yake Rais amefungua pia kiwanda cha kuchambua pamba wilayani Maswa ambapo pia amehutubia wananchi wa wilaya ya bariadi.