Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025.

Viongozi hao wamempongeza na kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa utekelezaji wa ahadi yake ya nyongeza ya mishahara, kupandisha madaraja ya watumishi wa umma na kuboresha mazingira ya kazi nchini.