Leo Jumanne, Februari 3, 2026, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameanza ziara ya kikazi hapa Dubai, UAE kwa kufanya mazungumzo na viongozi na wadau wa kimataifa.
Katika ratiba ya leo, Rais Samia anakutana na Mhe. Gaston Browne, Waziri Mkuu wa Antigua and Barbuda, pamoja na kufanya mazungumzo ya pande mbili na Bi. Shaikha Al Nuwais, Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UN Tourism), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha ushirikiano, diplomasia ya kiuchumi na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja nchini.
Jioni ya leo, Rais Samia atashiriki uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS)— jukwaa la uwekezaji linalolenga kuoanisha miradi iliyo tayari kuwekezeka barani Afrika na wawekezaji wa kimataifa.
GAIS ni mpango wa kimkakati unaoendeshwa sambamba na majadiliano ya sera ya World Governments Summit (WGS), kwa lengo la kubadili majadiliano ya sera kuwa uwekezaji halisi wenye matokeo.
Fuatilia kupitia akaunti rasmi za Ikulu Mawasiliano kwa taarifa zaidi.


