Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Julai 2025.
Rais Dkt. Samia anasafiri kwenda Umoja wa Visiwa vya Comoro kwa Ziara ya kikazi ya siku moja ambapo ni amealikwa kama Mgeni Rasmina na Rais wa nchi hiyo Mhe. Azali Assoumani kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa nchi hiyo zitakazofanyika kwenye Uwanja wa Malouzini Omnisport mjini Moroni.
