๐™‘๐™ž๐™Ÿ๐™–๐™ฃ๐™– ๐™ฅ๐™š๐™ฃ๐™™๐™š๐™ฃ๐™ž ๐™๐™–๐™ž๐™›๐™– ๐™ก๐™š๐™ฃ๐™ช, l๐™ž๐™ฃ๐™™๐™š๐™ฃ๐™ž ๐™ฃ๐™– ku๐™™๐™ช๐™ข๐™ž๐™จ๐™๐™– a๐™ข๐™–๐™ฃ๐™ž ๐™ฎ๐™– ๐™‰ln๐™˜๐™๐™ž ๐™ฎ๐™š๐™ฉ๐™ช.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. ๐—ฆ๐—ฎ๐—บ๐—ถ๐—ฎ ๐—ฆ๐˜‚๐—น๐˜‚๐—ต๐˜‚ ๐—›๐—ฎ๐˜€๐˜€๐—ฎ๐—ป amewasihi Vijana kutokubali kushikiwa akili na kushawishiwa katika kuichoma na kuiharibu nchi yao wao wenyewe kutokana na ushawishi wa watu wachache wenye kutanguliza maslahi yao binafsi na kutokuwa na uzalendo wa kweli kwa Taifa lao.

Akihutubia Bunge katika kulifungua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la 13, leo tarehe 14 Novemba 2025 Jijini Dodoma, Rais Dkt. Samia ameyasema haya;

โ€œPamoja na kuwa uchaguzi ulifanyika, kulijitokeza vurugu za uvunjifu wa amani ambao ulisababisha uharibifu wa mali, kupoteza maisha na kuhatarisha usalama wa Nchi”

“..tunapoenda mbele niwasihi sana Watanzania tuongozwe na dhamira ya maelewano, ushirikishwaji, kujirekebisha na umojaโ€

โ€œKwa Wanangu Vijana wa Taifa hili la Tanzania niseme kwamba nchi hii imejengwa kwenye misingi ya amani na utulivu wakisiasa, sisi Wazazi wenu kama tungeyafanya mliyoyafanya wakati huu Nchi hii isingekuwa na neema na maendeleo mnayoyaona leoโ€

โ€œNarudia hilo, kwa Wanangu Vijana wa Tanzania, sisi Wazazi wenu kama tungeyafanya mliyoyafanya nchi hii isingekuwa na neema na maendeleo mnayoyaona leo”

“..hivyo niwasihi sana Wanangu Vijana wa Taifa hili, nchi hii ni yenu kwa shida zozote zile zinazowakabili, msikubali hata siku moja kushawishishiwa kuichoma nchi yenu wenyeweโ€

โ€œMsikubali kukata tawi la nchi mliyoikalia msikubali kabisa, hili nawaomba mlikate kwa nguvu zenu zote , nyie ndio Wajenzi wa Taifa hili nawasihi kamwe msiwe Wabomoaji wa Taifa hiliโ€