Rais wa Jamhuri ya Namibia akisalimiana majirani zake wakati akiishi Magomeni Mikumi Jijini Dar es Salaam
JamhuriComments Off on Rais wa Jamhuri ya Namibia akisalimiana majirani zake wakati akiishi Magomeni Mikumi Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah akisalimiana na Bi. Salama Salehe Ghulum (Mama Salehe) na Bi. Rafran Ismail Khan ambao walikuwa majirani zake wakati akiishi Magomeni Mikumi Jijini Dar es Salaam katika miaka ya 1980s. Mhe. Rais Dkt. Nandi-Ndaitwah alikutana na jirani yake huyo wa siku nyingi katika hafla ya chakula cha jioni alichoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Mei, 2025.