Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam kwa kushirikiana na vyombo11 Agosti, 2025 wamefanikiwa kukamata Ramadhan Makala Mkazi wa Tabata kwa tuhuma za kusafirisha bangi gunia 13 zenye uzito unaokadiriwa kuwa kilogramu 239 kwa kutumia gari lenye usajili wa T. 733 AGT aina ya FUSO
ambapo magunia hayo yalikuwa yamechanganywa na mengine ya mchele
yakitokea Morogoro kuletwa Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam CPA Jumanne Muliro amesema mtuhumiwa wenzio watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Katika tukio lingine Agosti, Polisi ilifanya doria eneo la Magomeni Kinondoni
walikamatwa watuhumiwa mawili Hassan Hamis Mkazi wa Tandale na Elia Mapunda Mkazi wa Goba Njia nne wakiwa na pikipiki sita zenye usajili wa MC 283 EGQ aina ya Haojue, MC 826 EZQ aina ya Boxer,
MC 407 EUV aina ya Boxer, MC 523 ENF aina ya Boxer, MC 479 CYY aina ya Boxer, MD2B15BX2MWE97341 aina ya Boxer na vipuli mbalimbali vya pikipiki mali ambazo ni za wizi.

Kamanda amebainisha kuwa wahusika wanatuhumiwa kujihusisha
na mtandao wa wizi wa pikipiki pia wamekamatwa wanaojihusisha na makosa ya uvunjaji ambao ni Gift Shabani Mkazi wa Kimara, Hussein Ally Mkazi wa Tandale wamekutwa na televisheni ishirini na moja na Razaki Ramadhani Mkazi wa Manzese amekutwa na simu za aina mbalimbali kumi ambazo ni za wizi.

Sambamba na hayo kuhusiana na kuzuia makosa ya usalama barabarani Polisi Dar es Salaam 16 hadi 25 Agosti, 2025 ulifanyika msako na yalikamatwa magari 15 yenye namba za usajili usio rasmi wa ‘SSH 2530’ kwa kosa la kuendesha chombo cha moto bila kuwa na usajili rasmi kinyume na kifungu namba 13(i) cha Sheria ya Usalama Barabarani sura 168 ya mwaka 1973 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2023.

“Polisi Dar es Salaam imejipanga vizuri kuhakikisha waumini wanashiriki na
kusherehekea Sikukuu hiyo kwa amani na utulivu wazazi na walezi kuwa na uangalizi wa karibu kwa watoto wakati wa matembezi na mikusanyiko mbalimbali, pia nyumba na makazi zisiaachwe bila uangalizi wakati wa sherehe hizi.

Suala la usalama barabarani pia limesisitizwa kwa madereva wa vyombo vya moto na watumiaji wengine wa bar abara kuzingatia sheria ili kuepusha ajali.

Aidha Jeshi Polisi linawatakia sikukuu njema ya Maulid wananchi wote wa Dar es
Salaam ambao wana ungana na Watanzania wenzao.