Na Mwandishi wetu, JamhuriMedia
Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amewataka Katika hatua wafanyabiashara wadogo waliovamia na kufunga njia za kuingia sokoni kuondoa shughuli zao mara moja na kuziacha barabara wazi kabla ya Februari 8, ili kuruhusu upatikanaji rahisi wa soko hilo na kuimarisha usalama pamoja na mpangilio wa shughuli za biashara.
Agizo hilo amelitoa Leo February 6,2026 Jijini Dar es salaam Wakati akizungumza na Wanahabari ambao ametangaza February 8 Mwaka huu Rais kutakuwa na Ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye anakwenda kuzindua Soko la Shimoni Kariakoo
Wamachinga wote waliopanga bidhaa zao katikati ya Barabara zinazopitika Maduka ya Kariakoo kuondoka mara moja pasipo Kutumia nguvu
Hata Amesema tayari Ujenzi imeshakamilika taratibu zilizowekwa kuwa Wafanyabiashara walioondoka Hapo awali kurejeshwa zilishafanyika.

“Mnafahamu Soko letu la Kariakoo tunafanya Biashara na Mataifa Mbalimbali ikiwemo Kongo,Zimbabwe ,Burundi hivyo tukiziba Barabara zinazoruhusu Wafanyabiashara Kuingia kwenye maduka Makubwa tutakimbiza wateja
RC Chalamila amesema itakumbukwa Soko Kuu la Kariakoo liliungua Julai 10, 2021 usiku huku wafanyabaishara 224 wakipoteza bidhaa zao. Serikali haikuwaruhusu wafanyabiashara kurudi tena na badala yake ilianza mchakato wa ujenzi wa soko jipya na ukarabati wa jengo la zamani
Aidha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aloelekeza kiasi cha shilingi Bilioni 32.2, bilioni 6 zitatumika katika ukarabati wa soko la zamani la Kariakoo na zaidi ya Bilioni 26 zitatumika katika ujenzi wa soko hipya

