Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Said Mtanda,amesema hadi saa 6 na dakika 18,Desemba 9,2025,hali ya usalama mkoani humo ni tulivu huku akiwatoa hofu wananchi juu picha mjongeo ‘clip’, zinazotembea mtandao zikionesha wanajeshi wakiwasikiliza wananchi.
Mtanda amezungumza hayo leo Desemba 9,2025 ofisini kwake jijini Mwanza,amedai kuwa amekuwa akipata simu nyingi hivyo hawezi kujibiu simu moja moja.
“Kwa ujumla nataka niwahakikishie Watanzania na wananchi wa Mkoa wa Mwanza wawe na amani,hali ya utulivu ni kubwa sana,ninawatakia wananchi heri ya miaka 64 ya uhuru wa Tanganyika,na ninawashukuru kwa kuendelea kuitikia wito wa Serikali wa kuwataka kufanya kazi zao kwa amani na utulivu katika siku hii ya leo Desemba 9,2025,”amesema Mtanda na kuongeza kuwa:
“Huku wale ambao hawana majukumu mengi au dharura kuendelea kusalia nyumbani na kuendelea kufuatilia shughuli nyingine kupitia runinga na njia nyingine,”.
Mtanda amesema, muda mfupi uliopita ameona picha mjongeo”clip” ikizunguka katika mitandao ya kijamii inayoonesha kikundi cha wanajeshi kikiwasikikiza wananchi ambao wanatoa hoja mbalimbali.
Amewatoa wananchi hofu hali huku akisema kuwa hali ya usalama ya Mkoa huo ni tulivu huku akiwahakishia kuwa “clip” hiyo ilirekodiwa Oktoba 31,2025 baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
“Ili kuwa siku tatu baaada ya uchaguzi mkuu,ninapozungumza leo nikiwa katika ofisi yangu ya Mkuu wa Mkoa saa 6 na dakika 18,vyombo vyetu vya usalama vimenihakikishia,na mimi mwenyewe nimejiridhisha nimepita katika maeneo na mitaa mbalimbali nikiangalia baadhi ya wananchi wachache wakiendelea na shughuli zao,lakini hakuna mkusanyiko wowote unaoendelea wala hakuna taharuki yoyote katika mji wetu wa Mwanza,”amesema Mtanda na kuongeza:
“Clip hiyo ipuuzwe imepitwa na wakati, nafikiri inatumika kama propaganda katika kipindi hiki ili kuleta taharuki, Watanzania na wanamwanza kuweni na amani, nimetoka soko la samaki nimenunua samaki na ninaendelea na shughuli zangu na sasa naenda maeneo mengine kuangalia hali ya usalama na shughuli za wananchi,”.


