Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), ameongoza maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali, majeshi mengine pamoja na wananchi kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Songwe katika hafla ya kuuaga mwili wa Ex Sajenti Perpetua Mohamed Hassan.

Marehemu ni mke wa Kaimu Mkuu wa Polisi Wilaya ya Momba Mkoani Songwe, Mrakibu wa Polisi (SP) Bhoke Simango.

Ibada ya kuuaga mwili imefanyika nyumbani kwa marehemu, Nselewa, Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, ambapo mamia ya waombolezaji walikusanyika kutoa heshima zao za mwisho.

Katika Msiba huo, Viongozi mbalimbali wa Serikali walihudhuria msiba huo, wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Frank George Haule Hawassi. Pia alikuwepo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga, pamoja na wafanyabiashara, viongozi wa vyama vya siasa wakiongozwa na chama tawala, ndugu, jamaa na marafiki wakitoa salamu za pole na faraja kwa familia ya marehemu.

Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kuelekea Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara, kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika huko.