Mradi wa Rwanda wa zao la bangi kwa ajili ya matibabu ya thamani ya Juu (HVTC) unapiga hatua kubwa, huku mradi wa miundombinu ya matibabu ya zao hilo ukiwa umekamilika kwa asilimia 83, kulingana na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB).

Mradi wa bangi ni sehemu ya hatua ya Rwanda katika tasnia ya matibabu na dawa, kwa lengo la kuchangia utafiti wa afya ulimwenguni na uchumi.

Kampuni tanzu ya KKOG Global – King Kong Organics (KKOG), ilikwa ni kampuni ya kwanza kupata leseni ya miaka mitano kutoka kwa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB) kuendesha uzalishaji wa bangi.

Kampuni hiyo hapo awali ililiambia gazeti la The New Times nchini humo kwamba ilikuwa imefanya uwekezaji wa dola milioni 10 katika mashine, ujenzi wa kituo, malipo ya ada katika upatikanaji wa ardhi na wakandarasi, pamoja na kuagiza mbegu za bangi zilizobadilishwa vinasaba.

Kukamilika kwa shughuli za ujenzi wa kituo cha uzalishaji wa bangi, kilichoko katika Wilaya ya Musanze katika Mkoa wa Kaskazini, hapo awali kilikuwa kimepangwa kuhitimishwa ifikapo Mei mwaka jana kabla ya kuongezwa hadi Septemba mwaka huo huo.

Kulingana naye, mchakato wa uzalishaji ambao unahusisha uukamuliwaji wa mafuta ya bangi ambayo yatasafirishwa kwa masoko yaliyolengwa utawezekana kwa ushirikiano wa serikali ya Rwanda itakayochangia takriban dola milioni 3 katika mradi huo.

Rwanda tayari imetenga hekta 134 kwa kilimo cha bangi ya kimatibabu, hasa ikilenga mauzo ya nje.