Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Same

Washtakiwa saba wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Same jana Februari 19, 2026, wakikabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na dawa za kulevya aina ya mirungi, huku mmoja wao akiamriwa kuwa chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi kwa miaka mitatu.

Washtakiwa hao kila mmoja amefikishwa mahakamani hapo na kesi yake nankufanya idadi ya kesi hizo kuwa Saba, walisomewa mashtaka yao dhidi ya dawa za kulevya aina ya mirungi.

Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Christanta Chitanda ilisikiliza mashtaka ya washtakiwa ambayo ni, Athuman Kivuma, Goodluck Mungulu na Nuru Mndeme.

Upande wa Jamhuri ulidai katika kesi ya kwanza kuwa, Mungulu anakabiliwa na shtaka la kukutwa na mirungi yenye uzito wa kilo 1.8.

Mshtakiwa alikana shtaka hilo na alishindwa kutimiza masharti ya dhamana amerudishwa mahabusu hadi Februari 24,mwaka huu.
Kesi ya pili na ya tatu, inamkabili Kivuma anakabiliwa na shtaka la kusafirisha mirungi kilo 27 na Mndeme anatuhumiwa kusafirisha mirungi kilo 25.

Wakati huohuo washtakiwa wanne wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi ambao ni, Youze Kitua, Ahadi Mnjama na Edson Kibaja.

Katika kesi ya nne, ya Tano na ya sita Kitua anakabiliwa na shtaka la kusafirisha mirungi kilo 34, Mnjama anatuhumiwa kusafirisha mirungi kilo 26 na Kibaja anakabiliwa na shtaka la kusafirisha mirungi kilo 24, walikama mashtaka yao na kesi zao zotatajwa Machi 3, mwaka huu.

Kwa upande wa kesi ya saba, mshtakiwa Mganga Dorovu upande wa Jamhuri uliomba kimweka chini ya uangalizi, mahakama imekubali na imeamuru kumweka chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi na kuwa na tabia njema (binding over).

Mahakama iliamuru awe chini ya uangalizi wa Polisi Same kwa kipindi cha miaka mitatu na kuripoti kituoni kila mwezi, kwa masharti ya kutojihusisha na uhalifu wowote, ikiwemo biashara au matumizi ya dawa za kulevya.

Hatua hiyo inaendelea kuonyesha juhudi za vyombo vya dola katika kukabiliana na biashara na usafirishaji wa dawa za kulevya katika Wilaya ya Same na maeneo jirani.