Na Kulwa Karedia, Jamhuri Media, Moshi
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema kama atapewa ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha anajenga Kampasi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Akihutubia mamia maelfu ya wananchi wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Oktoba mosi, Rais Samia amesema ametekeleza vizuri ahadi za ilani iliyopita na ijayo itakuwa zaidi.
Tujenga chuo hiki ili kuleta karibu fursa za juu za mafunzo ya biashara, chuo hiki kitaimarisha uchumi wa eneo husika, vijana wetu wengi watapata nafasi ya kusoma.
Kwa umeme wa kule vijijini gharama za halisi za kuunga umeme kwa mwananchi wa kawaida ni shilingi 400,000, lakini serikali imesema watu wa vijijini wataunganishwa kwa shilingi 27,000 tu, ndiyo maana serikali inabeba gharama zingine, hii ni ruzuku.
Tunapokuja kwenye nishati safi ya kupikia, gharama ya mtungi wa gesi mnaujua, serikali imesema ni shilingi 16000 kwa maeneo yaliyochaguliwa, hii nayo ni ruzuku kwa wananchi wa Tanzania, kwa hiyo pamoja na haya yapo mengi ambayo yanawapa nafuu ya maisha wananchi wa Tanzania,amesema.
Amesema katika mkoa wa Kilimanjaro kumetokea mambo makubwa na mazuri yalioyofanywa na serikali kwa kushirikiana na taasisi binafsi.
Tumefanya maboresho makubwa katika hospitali ya mkoa ya Mawenzi, nakumbuka nilikuja mwenyewe kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la kina mama na watoto ambalo sasa limekamilika na kuanza kutoa huduma.
Uwezo wa jengo lile umewezesha kina mama wengi kwenda kujifungua kwenye hospitali mbalimbali.
Mwitikio wa kina mama kwenda hospitali ndani ya mkoa sasa ni kutoka 260486 hadi 328502 kwa kiasi kikubwa tumepunguza vifo vya kina maama wakati wa kujifungua na jitihada hizi zitaendelea kila wakati, zaidi hospitali yetu ya rufaa ina huduma za wagonjwa mahututi na watoto njiti, kufisha fugo huduma ambazo awali hazikuwapo.
Tuweka vifaa vya kisasa vya vipimo kama CT SCAN, X-ray inayomfuata mgonjwa na siyo mgonjwa anaifuate, kama uko kitandani inakuja hapo hapo,pia huduma za MRI sasa Kilimanjaro imejitosheleza mno. Kwa kushirikiana na hospitali za kidini kama KCMC tumefanikisha kujenga banka la mionzi ambalo litakuwa linatoa tiba ya maradhi ya kansa, hakuna haja kwenda Dar es Salaam,amesema.
Amesema katika miaka mitano ijayo huduma hizo zitaendelezwa na hivi sasa wanakwenda kukamilisha maboresho ya hospitali za Moshi, Mwanga na Rombo kwa kuongeza watumishi, vitendea kazi na vifaa tiba pia upatikanaji wa dawa.
Upatikanaji wa dawa tumeutoa ulipo sasa ni asilimia 86 kitaifa na tutahakikisha dawa muhimu lazima zinapatikana.
Kuhusu mradi wa Same-Mwanga-Korogwe, Rais Samia anasema umekamilishwa awamu ya kwanza na maji yameanza kupatikana, sasa anajianda na awamu ya pili ambayo itagusa vijiji vya Same na Mwanga na majirani zao Korogwe.
Pia tumeendeleza miradi mingine ya maji ambapo katika Wilaya ya Hai tumekamilisha mradi wa maji kutoka Uroki-Bomangombe kwa gharama ya Sh bilioni 300.9, Rombo tunatekeleza mradi wa shilingi bilioni 9.8 kutoa maji ziwa Chala, tunategemea kutumia maji maeneo mserereko kufikisha huduma kwa wananchi kule Longai na Marangu.
Kwa upande wa Wilaya ya Siha, tunatekeleza mradi wa shilingi bilioni 14 kupeleka maji kwenye vijiji vinane na kote kazi inaendelea lengo letu ni kila mwananchi awe karibu na huduma ya maji safi na sala,a,amesema.
Kuhusu elimu anasema serikali itaendelea kutoa elimu bila malipo, kujenga shule za msingi, sekondari pamoja na VETA.
Kwa upande wa umeme, Rais Samia anasema serikali imefanya kazi nzuri mno kwa sababu vijiji vyote alivyopita miundombinu ya umeme pamoja na barabara.
Mengi yamefanyika kwenye sekta ya barabara, ikiwamo kazi kubwa tuliyofanya kurekebisha maeneo mengi kutokana na athari za mvua kubwa ambazo hujitokeza. Hapa Moshi mjini kama tulivyoahidi tutajenga barabara mchepuko (bypass), ya Kahe- Uwanja wa ndege yenye urefu wa kilomita 31, tumekwisha weak fedha za urefu wa kilomita 17 ndani ya mpango wa tactic.
Tumekamilisha barabara za Nation School-Kibosho Kati- Kwa Raphael kwa urefu wa kilomita 15, pia barabara ya Mamboleo-Shimbwe yenye urefu wa kilomita 10.3 na Mamboleo-Kiteruni yenye urefu wa kilomita 10, barabara ya Samanga-Chemchem yenye urefu wa kilomita 10 zote hizi zinajengwa na ziko kwenye hatua mbalimbali zitakamilishwa kwa kiwango cha lami,amesema.
Kwa upande wa Jimbo la Vunjo, amesema watakamilisha barabara ya Pofa-Mandaka-Kilema yenye urefu wa kilomita 10 ambayo inategemewa na wananchi kufika katika hospitali za Kilema, Chuo cha Mandaka na geti la watalii wanaoshuka mlima Kilimanjaro.
Huko huko Vunjo kuna barabara ya Kisomachi-Uchila-Kwararia yenye urefu wa kilomita 10.8, kilichotofautisha mradi huu na mingine ni kuwa wananchi walianza kwa nguvu zao na baadae serikali ikaingia,amesema
Kwa upande wa Same, Rais Samia anasema kuna tatizo kubwa hasa maeneo ya milimani wakati wa mvua wananchi wanapata shida kushuka maeneo ya tambarare. Hivyo serikali inakwenda kuzifanyia uchunguzi kisha zijengwe kwa kiwango cha lami na zege.
Nawapongeza Kilimanjaro kwa maendeleo makubwa haya ambayo mmefikia,nisisahau kule Rombo tutakamilisha ujenzi wa barabara ya Horiri-Tarakea yenye urefu wa kilomita 53 ambayo ni ya kimkakati wa kukuza biashara na majirani zetu wa Kenya, itapunguza msongamano wa magari ya mizigo kule Mwika-Tarakea.
Nafahamu sana wananchi wa Moshi Vijijini ni wakulima wa kahawa, tunapokwenda mbele pamoja na kuleta pembejeo za ruzuku tutaanzisha vituo vya kukodisha zana za kilimo ili kuwawezesha wakulima kwa gharama nafuu zaidi. Kama navyosema kote tuna mpango wa kuleta matrekta 10,000 yatakpoeshwa na kuuzwa kwa wakulima nchi nzima,amesema.
Kuhusu wafugaji, Rais Samia anasema serikali imejenga majosho Siha na Hai,huku wakitoa ruzuku ya chanjo kwa mifugo.
Mkitupa ridhaa ahadi yetu ni kuongeza maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wafugaji kutoka ekari milioni 3.6 hadi milioni 6, huku ndiko wafugaji wetu wakapofuga kisasa sana kwa kupanda maji ili ngombe wale pamoja, tumefanya kazi kubwa ya kukuza eneo hili,amesema.
Kuhusu utalii, anasema umekuza uchumi kwa kiasi kikubwa mno kwa kuongeza watalii, fursa za ajira, kipato na kufungua ajira nyingi kwa vijana.
Tumekuza idadi ya watalii kama tilivyoweka kwenye ilani yetu wafikie milioni 5, sasa lengo letu ni kufikisha watalii milioni 8 kwa mwaka,amesema
VIWANDA
Kuhusu viwanda, Rais Samia anasema miaka ya nyuma mji wa Moshi ulikuwa na viwanda vingi ambavyo baada ya ubinafishaji vilishindwa kuendelea na kukosesha vijana wengi ajira.
Hii ni changamoto maeneo mengi ya nchi, hivyo ahadi yetu kwa nchi nzima tutahakikisha viwanda hivi vinafanya kazi kwa kuwatafuta waendeshaji wengine, vikiwamo vyama vya ushirika kwa sababu tumevijenga kiasi ambacho sasa vinaweza kusimama na viwanda kuendesha.
Viwanda kama vya chai mkoa wa Tanga tutakabidhi kwenye vyama hivi, tukiona vingine wanaweza tutawapatia na kutafuta wawekezaji wengi.
Hapa Moshi tumefufu kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools kilichokuwa kimesimama kwa zaidi ya miaka 30, tayari kinatoa huduma kwa kutengeneza vifaa (spear parts). Tupeni nafasi tutaimarisha kiwanga hiki kitafuata malighafi ya chuma na makaa ya mawe, hili tunalisema kwa uhakika,amesema.
Miradi mingine ya kimkakati ni ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Tanga- hadi Musoma itapita hapa Moshi-Arusha, mradi huu utatoa ajira na kuchochea biashara na uchumi.
HAI
Akiwa eneo la Bomangombe wilayani Hai, Rais Samia amewahimiza wananchi kutokubali kushawishika na kufanya fujo zitakazoharibu amani ya nchi.
Amesema ni vizuri Watanzania wakatambua gharama ya amani ya taifa iliyopo na si kila mtu anafurahia kuona hali hiyo ya kuwa kisiwa cha amani.
Naomba mno msikubali kushawishiwa kuharibu amani ya Tanzania.
Msikubali hata kidogo hawa wanaotaka kufanya hayo wana mahala pa kukimbilia, likitokea jambo wanataka tuwarudishe uwanja wa ndege na hatia zao za kusafiria wanaondaka familia zao hazipo hapa, tunakwenda wapi, tusikubali.








