
Na Mwandishi Wetu, Jamhuri Media-Uyui
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Samia Suluhu Hassan amewataka wafuasi wa Chama kuvunja makundi mara ili waende kwenye uchaguzi mkuu wakiwa wa moja.
Rais ametoa kauli hiyo katika Kijiji cha Ilolangula wilayani Uyui mkoani Tabora wakati wa mkutano wa kampeni leo Septemba 11,2025.

“Ndugu zangu chama chetu kmekwishapata wagombea ule mchakato wa wa uteuzi umekwisha, nawaomba tuvunje makundi yote twende kwenye uchaguzi tukiwa wa moja.
“Sifa ya CCM ni kurudi kuwa chama kimoja, twende kwenye uchaguzi tukiwa na nguvu moja tu,”amesema.
Amesema lazima uwepo umoja na mshikamano ndani ya Wilaya ya Iyui kwa ajili ya ustawi wa chama hicho.



