Na Kulwa Karedia, Jamhuri Media, Sengerema
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amesema wapo Watanzania ambao kila wakiona jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaheshimika duniani kazi yao wao ni kushusha heshima ya nchi yao.
Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati wakihutibia maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Sengerema kwenye uwanja wa Mnadani mkoani Mwanza wakati wa mkutano wake wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani Oktoba 7, 2025.
Wapo Watanzania ambao wakiona jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa na kazi ya kushusha heshima yake, hao naomba tuachane nao, waacheni waende kivyao vyao, hao siyo wenzetu hata kidogo.

Ili kuheshimisha nchi yetu tufanye uchaguzi kwa amani bila vurugu, bila kuvunja utaratibu, tutaheshimisha nchi kama tutafuata haki kila mtu anaipata. Nje ya nchi ni kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ambao mpaka hatua iliyofikia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaheshimika sana, haya ndo mambo ambayo mkitupa ridhaa tunakwenda kuyaendeleza pamoja na mambo yote ya maendeleo,amesema.
Amesema anataka kuona kila Mtanzania yuko karibu na huduma za afya, napata majisafi na salama, anapata nishati ya kutosha ya kutumia kwa maendeleo yake.
Amesema chama hicho kina ajenda kuu tatu ambazo zimebeba maoni ya Watanzania katika Ilani ya mwaka 2025-30.
Ajenda ya kwanza ni maendeleo ya jamii, tunapozungumzia hii ndipo Watanzania wetu wanapara maji safi na salama, umeme, elimu na baraabara. Sekta hizi tumezifanya vizuri sana.

Ajenda yetu ya pili ni maendeleo ya uchumi, hapa tunazingalia sana sekta za kilimo,uvuvi, ufugaji na madini. Ndiyo maana kwenye kilimo na ufugaji, serikali tumejitoa mno kutoa ruzuku na pembejeo ili sekta hizi zikuwa na zilete ajira, mapato kwa watu wetu, uchumi imara kwa watu wetu,ajira kwa vijana ndiyo maana tunaleta pembejeo za kilimo kwa ruzuku ili mazao yetu yawe kiwango kibora na wakulima wafaidike,amesema.
Amesema Watanzania ni mashahidi kwa sababu suala hilo limefanyika kwa ustadi mkubwa katika maeneo mbalimbali nchini kwa sababu uzalishaji wa mazao ya kilimo yameongeza ndani ya miaka minne.
“Hatukuishia hapo, nikutafuta masoko bei zinazolipa jasho la mkulima na hilo tumefanikiwa, lakini biashara mwaka huu wakati mwingine bei zinakuwa juu mwaka mwingine zinashuka kidogo.
Tumejitahidi sana kuunganisha ncho yetu na masoko ya dunia ili tunapozalisha tunakwenda kwenye masoko ya dunia tunafanya mnada wakulima wanashuhudia mazao yetu yanavyouzwa,amesema.

Amesema kwenye kilimo, serikali imefanya kazi kubwa ya kujenga maghala na vihenge vya kutunzia mazao yakiwamo ya biashara na chakula.
Siku hizi hakuna mazao ya biashara au ya chakula yote yakiwamo mahindi, mbaazi au choroko yote haya ni ya biashara. Kuhusu uvuvi ndiyo maana tumeweka nguvu kubwa mkoa huu tumeleta boti na mikopo kwa wavuvi, tumejanga vizimba 400 vya kufugia samaki.
Pia kuhakikisha viwanda vya kuchakata samaki vinaendelea kufanya kazi ili vijana wazalishe, ziwa lizalishe ili tukipeleka kiwandani tunapata fedha ya kutosha,amesema.

Kuhusu ufugaji, Rais Samia amesema Tanzania imefanikiwa kupata soko kubwa la mauzo, kibaya tulikuwa tunakwamishwa eti nchi yetu haimo kwenye orodha ya dunia ya nchi ambazo zinachanja wanyama wake.
Tumeleta chanjo za ruzuku unalipa nusu kwa mifugo ya ngombe, kondoo, mbuzi kila mmoja ana bei yake, kwa kuku tumesema ni bure, lengo ni kuiweka nchi yetu kwenye orodha ya dunia ili tujulikane tunachanja, tunatambua mifugo yetu, tukiweka vizuri jambo tuna soko kubwa ambalo hatuwezi kulimaliza huko ndiko Tanzania inakoelekea,amesema.
Amesema sekta hizo tatu lazima zizalishe viwanda vya kuwekeza samaki, iwe uvuvi lazima kuwepo na viwanda vidogo vidogo vingi ambavyo vitasaidia kutoa ajira kwa vijana na kuongeza thamani.
Jambo hili tumeliweka kwenye Ilani yetu kwamba kila wilaya itakuwa na viwanda vya kuongeza thamani mazao yanayozalishwa wilaya husika.Suala jingine kwenye uchumi ni usafiri uwe wa barabara, maji, anga au reli kote serikali yenu tunapafanyia kazi,amesema.

Amesema katika ilani ya 2025030 kuna reli za aina tatu ambazo wanashughulikia, reli itakayofungua ukanda wa kusini, kaskazini na SGR inayokwenda Dodoma na TAZARA nayo inakwenda kufanyiwa marekebisho makubwa.
Amesema serikali imelifufua na kuliimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATC) kwa kununua ndege za kisasa ambazo sasa zimefika ambazo zinafanya safari zake ndani na nje ya nchi.
Amesema Tanzania imezungukwa na nchi nane ambazo zote zinaitgemea katika mambo mbalimbali yakiwamo ya chakula.
Hivi tunavyozungumza maparachichi ya Tanzania, mchele uko Ulaya, tuwekeze uzalishaji zaidi ili tupate biashara,amesema.


