Na Kulwa Karedia, JamhuriMedia, Geita

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amemwaga neema ya mambo muhimu mkoani Geita ambayo ameahidi kuyatekeleza endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.

Neema hiyo ni pamoja na ujenzi wa maabara ya kisasa ya kuchakata dhahabu mkoani Geita, kuanzisha viwanda vya kuchakata alizeti, ujenzi wa uwanja wa ndege mjini Geita na uwanja wa michezo.

Akihutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Geita wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais,wabunge na madiwani kwenye uwanja wa Bombambili Oktoba 13, 2025.

Napenda kuwambia tunakwenda kujenga maabara ya kisasa ambayo itasaidia kurahisisha kazi za wachimbaji iishie ndani ya mkoa badala ya kufuata huduma hiyo mbali.
Tunajiandaa kutoa mitaji kwa wachimbaji wadogo kuwakuza ili wawe wakubwa, kuongeza maeneo mapya ya uchimbaji na kupimza zaidi nchi yetu ili kubain madini zaidi yako wapi na ya aina ili uchimbaji ukuwe zaidi,amesema.

Amesema serikali imejipanga kuanza ujenzi wa majengo ya kisasa yatakayotumika kwa ajili ya mikutano ya kitaifa ya masuala ya madini katika viwanja vya Bombambili.

Tutajenga majengo ya kimataifa ili mikutano ya kimataifa ya madini ifanyikie hapa hapa na uwanja wa maonyesho, badala ya kufanyika Dar es Salaam au kwingine,amesema.

Amsema mkoa wa Geita umekuwa na maendeleo makubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012.

mkoa huu ni mchanga, lakini umedhihirisha uimara katika ukuwaji wa uchumi, ustawishaji wa jamii ukizingatia nguzo kuu za maendeleo za mkoa huu ni madini, kilimo na ufugaji.

Katika kipindi hiki cha miaka mitano tunachomalizia jitahada za serikali zilielekezwa kwenye masuala ya jamii, ujenzi wa miundombinu na mipango ya kuwezesha wananchi.

Matokeo ya jitihada za pamoja kati ya serikali na wananchi matokeo yanaonekana dhahiri, kwani sasa Geita kuna ustawi mkubwa zaidi kwani hata makazi ya watu yameboreshwa sana, Geita nayoifahamu ya mwaka 2015 si hii ya leo, hongereni sana,amesema.

Amesema Ilani ya chama hicho imeelekeza serikali kutekeleza mambo mbalimbali ambayo yamegawanyika katika mafungu matatu.

Fungu la kwanza, kuimarisha sekta za kimageuzi za uzalishaji kama vile kilimo, ambapo mmesikia waziri mwenye dhamana ameelezea vizuri sana, lengo letu ifikapo mwaka 2030 tunataka kilimo kiwe kimefika asilimia 10 na ichangie vema kwenye pato la taifa tukitambua ukuzaji wa uchumi wa wakulima wetu,amesema.

Amesema pia wameelekezwa kwenye sekta ya ufugaji ambayo serikali imefanya kazi kubwa na badi kazi inaendelea ikiwamo kuchanja mifugo, kujenga mabwawa, majosho na machinjio ya kisasa.

Amesema suala la tatu ni ujenzi wa ujenzi wa uchumi wa viwanda na kukuza biashara na fursa za ajira kwa vijana.

Hili tukilitafsiri kwa hapa mkoani, tunakwenda kuanza na ujenzi wa wa viwanda vya kuchaka mbegu za alizeti katika maeneo ya Busanda na eneo la Nyakamwaga na Sungusira kutajengwa kiwanda cha kusindika matunda.

Kitaifa tunataka kukuza sekta ya viwanda kutoka ukuaji wa asilimia 4 ya sasa hadi 9 mwaka 2030, kwa upande wa sekta ya madini ni moja ya kichecheo cha ukuajia uchumi,amesema.


Katika sekta ya usafirishaji, Rais Samia amesema serikali itaendelea na ujenzi wa barabara, ukiangalia ilani zetu ndogo kifungu cha 41 (a)mpaka G kinataja barabara zote zitakazojengwa ndani ya mkoa huu.

Amesema wametakiwa pia kujenga uwanja wa ndege kwenye maeneo mawili, kwanza kuuendeleza uwanja wa ndege wa Chato na pili kujenga uwanja mpya wa ndege katika mji wa Geita.

Kuhusu masuala ya vivuko, tumejipanga maeneo yote ya vivuko ndani ya mkoa huu tutajenga miundombinu na kuweka vivuko vyenye usalama viweza kuvusha watu. Eneo jingine ni nishati ambapo titajenga kituo cha umeme ili kuhakikisha ndani ya mkoa unapatikana muda wote bila kupungua ili ukafanye kazi kwenye viwanda.

Mbali na hayo, tutamalizia ngwe yetu ya umeme kwenye vijiji na vitongoji hadi kwenye visiwa ambavyo viko maeneo ambayo yana mahitaji haya,amesema.

Amesema kwa upande wa maliasili na utalii, kwa mkoani humo serikali itaendelea hifadhi ya Burigi- Chato na Hifadhi ya Lubondo pamoja na kudhibiti wanyamapori wahalibifu wanaokwenda kuharibu mashamba na kuzuru binadamu.

Eneo jingine ni matumizi endelevu ya ardhi katika hili tunakwenda kuangalia changamoto zinazokabili wakulima na hifadhi zetu na maeneo mengine, kubwa zaidi ni kupima na kumilikisha, tunapima maeneo ya wafugaji kutoka ekari milioni 3.4 mpaka milioni 6, tutapima miji ya makazi na maeneo ya uwekezaji.

Eneo la pili kuboresha maisha ya watu na ustawi wa jamii ambapo kwa mkoa huu tulianza vizuri sana na tumeanza katika huduma za afya kwa kujenga hospitali za kibingwa na matibabu bobezi, tumejenga hospitali za rufaa.

Sasa hivi ndani ya mkoa huu mambo yote yatamalizika humu humu si kwa maradhi ya kawaida, lakini hata moyo tunajenga tawi la Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI), matibabu hapa hapa hii itasaidia mikoa jirani na wenyewe watakuja kupata huduma. Naamini hata nchi jirani zitakuja hapa hapa, pale Chato kuna hospitali kubwa ya rufaa ya mkoa ambayo itatoa matibabu ya kawaida na kibingwa.

Tutaendelea kujenga zahanati na vituo vya afya kwa maeneo ambayo hayana huduma hizi. Kwa hapa mjini tunaendelea kuboresha hospitali ya wilaya tutajenga jengo la upasuaji na la kuhifadhia maiti, pia vituo katika maeneo ya Mgusu, Bulela na Mtakuja pamoja na zahanati 12 na kufikisha idadi ya zahanati 26,amesema.

Kuhusu elimu, ameanza serikali imeanza vizuri kwa kujenga shule za msingi, sekondari na vyuo vya veta ili kufundisha vijana masuala ya ufundi kwa ajili ya kujiajiri.

Kuhusu ombi la kupata tawi la chuo kikuu, Rais Samia amesema tayari wameanza ujenzi kampasi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), ambapo ujenzi wake utagharimu Sh bilioni 11.