Na Kulwa Karedia,JamhuriMedia-Zanzibar
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amesema muungano wa Tanngayika na Zanzibar umeimarika zaidi tofauti na miaka yote.
Amesema Muungano huo sasa na udugu wa damu, huku akiwanyo wale wote ambao wamejipanga kuvuruga amani kwa kusema vyombo vya dola vimejipanga vema kudhibiti lolote litakalojitokeza.

Akihubumia mamia ya wafuasi wa chama hicho katika viwanja vya Kajengwa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja Septemba 17, 2025, Rais Samia amesema utulivu wa kisiasa ni muhimu ndani ya nchi kuliko kitu chochote.
Tumejinpanga vizuri ili kulinda heshimwa ya wasisi wetu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume tangu mwaka 1964, tumeweza kuenzi Muungano wetu, mafungamano kati yapande zote mbili yameendelea kukuwa, yamekuwa kifamilia, kijamii, kibiashara, kisiasa na kiuchumi ambao ndiyo ulikuwa msingi wa muungano wetu.
Tumeweza kuukuza katika nyanja zote hizo, naweza kusema sasa umekuwa Muungano wa udugu na damu zaidi kuliko vigezo vingine vyote, pamoja na mambo mengine tumeweza kulinda uhuru na mapinduzi matukufu ya Zanzibar, kudumisha amani, tulivu na umoja nchini,amesema.

Amesema hizo ndiyo tunu kuu na za msingi kwa maendeleo ya taifa, zitalindwa kwa bidii zote na kubwa
Tunakwenda kulinda tunu ya Muungano, amani, utulivu na ndani ya nchi yetu. Sifa hizi ndiyo zimejenga taifa la Tanzania na utambulisho wa kipekee kikanda na kimataifa, umekuza uhusiano wa kidplomasia na kufanya kuwa mbia muhimu wa kutegemewa sana duniani,amesema.
Amesema hatua hiyo imefungua ushirikiano na fursa za zaidi kwa Watanzania na hivi sasa huko duniani wanatambea kifua mbele.
Hivi sasa ukitaja Tanzania mtu anakuuliza Mama Samiandiyo, taifa linajulikana. Hivyo basi katika jitihada za kuhifadhi urithi na kujenga uelewa kwa vizazi vya sasa na vijavyo tunakoendelea mbele na kutupa ridhaa tunakwenda kuanzisha kituo cha kumbukumbu na nyaraka za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kituo ambacho kitasadia vijana wetu na watu wote wanaotoka nje waingie wajue muungano una maana gain, umeanzaje na tunaundeleza vipi,amesema.

Jambo jingine ambalo ameligusia ni suala la kitulivu wa kisiasa na amani ya nchi.
Tunaingia kipindi cha uchaguzi, mwanzo nilipokuja kujitambulisha ahadi kubwa niliyoitoa kwenu ni kuifanya Tanzania iwe na amani na utulivu, nilipotembelea kisiwa cha Pemba, kubwa nililoombwa na wazee kule kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu na hili ndilo nalotaka nilitilie mkazo.
Tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu kwenye nchi yetu, ninawaomba sana twende tudumishe amani na utulivu, uchaguzi si vita, uchaguzi ni tendo la kidemokrasia, ni watu kwenda kwa utaratibu uliowekwa kuweka kura zetu rudi nyumbani katulie ili nchi ibaki salama. Sasa si muda wote kushika silaha kuna leta suluhusho.
Muda wote kushika silaha yoyote iwe ya moto au ya mila na kijadi haileti suluhisho, nawaomba ndugu zangu wote wanaotusikiliza amani na utulivu wa wan chi yetu ni jambo la muhimu zaidi kuliko jambo jingine lolote, nataka niwatowe hofu ndugu zangu Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vile vya Zanzibar vimejipanga vema kulinda nchi yetu, sasa hutaki kishindo rudi nyumbani tulia, tumejipanga vema,amesema.
Rais Samia alitumia fursa hiyo kumpongeza mgombe urais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pamoja na viongozi wote kwa kuzindua kampeni kwa kishindo kikubwa Jumamosi uliyopita.

Kwa kweli nimeona kampeni zimeanza vizuri sana, kama ilivyokuwa kule Bara, huku mmeamua kuzima zote na kuwasha
kijani.Mniruhusu nipongeze pongezi zangu nyingi pamoja na serikali yake kwa kazi kubwa ambayo imefanyika Zanzibar kwa kutekeleza Ilani ya CCM 2020-25, sote ni mashahidi kwa kazi kubwa iliyofanyika kila sekta kama ilivyoelezwa na wengine walionitangulia.
“Nakumbuka siku za nyuma kidogo, Dk Hussein alibandikwa jina la Mzee wa mabati, lakini wakati kulikuwa na ujenzi wa hospitali, shule, masoko na nyumba za kuishi, mahakama mambo yalikuwa mengi sana, sasa kwa sehemu kubwa mabati yale yameondoka tumeona kilichotokea, badala ya mabati mkasi uliongea.
Na mimi ni shahidi nilikuja kuongelesha mkasi kule kisiwani kwenye ile hoteli kubwa ya kitalii, nami nilikuwa shahidi pia, kila mmoja alijionea kazi kubwa iliyofanyika hapa Zanzibar. Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni, sasa Dk Mwinyi nisema msimyonge lakini haki yake apewe na maua yake apewe,amesema.
Amesema ni jukumu la wagombea wote sasa wanaogombea ubunge, uwakilishi na madiwani kupita kueleza yale yote yalifanyika na kutendeka ili watu wajaue na kuchagua chama hicho kutokana na kwamba CCM ndiyo inaleta maendeleo.

Ndugu zangu wagombea ubunge, uwakilishi na madiwani mna kazi ya kufanya, mnaposema mtakwenda nyumba kwa nyumba mtaaa kwa mtaa hii ndiyo kazi ya kwenda kueleza yaliyofanyika na kuomba kura kwa chama chetu.Tunapozungumzia mafanikio yanayotokana na Ilani hapa Zanzibar ndiyo ilivyo kote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo maana tumejiamini tumepata ujasiri wa kurudi tena kwenu ndugu wananchi, kuomba ridhaa ya kuongoza nchi yetu kwa miaka mingine mitano ili tuipeleke kwenye mafanikio makubwa zaidi,amesema.
CCM tumeweza, tumefanya, tuliahidi, tukatekeleza, tunaahidi makubwa zaidi tutatekeleza, tunajiamini na tuna kila sababu ya kuja kwenye kwa ujasiri kuwaambia tunawez tupeni, tutatekeleza,amesema.
Amesema mambo ambayo CCM imejipanga kuyafanya kwa miaka mitano ijayo kwa upande wa Zanzibar na Bara yalielezwa vizuri na Dk. Mwinyi vizuri siku ya uzinduzi wa kampeni Septemba 13, mwaka huu.

Nami mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mgombea mwenza, ndugu Emmanuel Nchimbi tangu tuzindue kampeni tumeendelea kupita maeneo mbalimbali ya nchi kukutana na wananchi kuwalezea mipango yetu na kuwaomba kura katika uchaguzi mkuu ujao, sasa ni zamu ya Zanzibar.
Wanasema sadaka huanza nyumbani si ndiyo, lakini na baraka zinapatikana nyumbani ndiyo maana nimeamua kuanza na uwanja wa nyumbani, nimekuja Makunduchi uwanja wa Kajengwa kuomba baraka za nyumbani, nimeanza na uwanja wa nyumbani, naomba baraka ili niweze kufanya yale yanayonikabili miaka mitano ijayo, nilipokwenda nilirudi kuomba baraka, nawashukuru sana wazee wangu wa Mkoa wa Kusini na nyumbani hapa walinipa baraka zimenisaidia kufanya vizuri sana, leo nimerudi tena, nazunguka Tanzania kuomba niaminiwe tena ili nikifanye makubwa ya yaliyopita.
Ndugu zangu kama nilivyoeleza tutaendelea na ushirikiano kati ya serikali zetu mbili, Seriakali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,amesema.
