Na Kulwa Karedia, JamhuriMedia,Mwanga
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameseama serikali imetenga Sh bilioni 1.9 kwa ajili ya ununuzi wa mitambo ya kuondoa magugu maji Ziwa Jipe lililopo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akituhubia wananchi wa wilaya hiyo wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu leo Septemba 30,2025.
Tumetenga shilingi bilioni 1.9 kununua mitambo ya kuondoa magugu maji yanayotishia uhai wa ziwa lile, tunategemea mitambo mitambo hii tutaipokea ndani ya miezi michache ijayo, tutaitumia hapa Ziwa Jipe na maziwa mengine ndani ya nchi yetu,amesema.




