Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan anatarajia kuendelea na kampeni zale cha uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani mkoani Septemba 28,2025.

Rais Samia kesho anatarajia kuhutubia mkutano mkubwa katika uwanja wa Sabasaba mjini Kibaha, baadae atakwenda Chalinze Msata ambako anasubiliwa kwa shauku na wana CCM wa maeneo hayo.

Rais Samia ana kampeni hizo katika uwanja wa Sabasaba mjini Kibaha baada ya kuhitimisha kwa kishindo kampeni katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi ambako aliahidi mambo mbalimbali kuyafanyia kazi endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa na kuongea nchi tena.

baadhi ya ahadi hizo ni pamo na kuwekeza katika teknolojia ili kuongeza ufanisi katika sekta mbalimbali za maendeleo,kuboresha sekta ya elimu kwa kuajiri walimu wa kutosha, hususan wa sayansi na hisabati,kutekeleza mradi mkubwa wa maji wa Nakonde ambao utasaidia wilaya za Mtwara Vijijini na Nanyamba.

Pia Rais Samia aliahidi kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuendeleza ruzuku za pembejeo kama salfa kwa wakulima wa korosho.

Ahadi nyingine ambayo amesema ataishughulikia zaidi ni kutatua migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji kwa kupima na kupanga matumizi ya ardhi, kutoka hekta milioni 3 hadi milioni 6 ifikapo 2030.

Amesema ataboresha
sekta ya afya kwa kupeleka vifaa tiba vya kisasa na kuajiri wataalamu wa afya ndani ya siku 100 za kwanza.

Ahadi nyingine ni ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Mtwara mpaka Mbambay Bay mkoani Ruvuma, kujenga reli ya Lindi Kusini, chuo cha uvuvi Kilwa pamoja na uchimbaji gesi asilia LNG.