Na Mwandishi Jamhuri Medii-Songea
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan Septemba 21,2025 atawasili mkoani Ruvuma kwa ajili ya mikutano ya kampeni.
Rais Samia anawasili hapa baada ya kukamilisha mikutano kama hiyo mjini Zanzibar.
Taarifa zinasema Septemba 21 atafanya mkutano mkubwa katika viwanja vya VETA mjini Songea ambako atanadi sera kwa wakazi wa mji huo.
Kampeni za Samia mkoani zinasubiriwa kwa hamu kubwa, maana kila kona ya imepambwa na rangi ya kijani na njano.
Hii ni sehemu ya kampeni rasmi za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ambapo Rais Samia anatafuta ridhaa ya kuendelea kuiongoza Tanzania kwa awamu nyingine.
Pia mgombea atafanya kampeni wilaya za Nyasa na Mbambay pia mkutano huo utahudhuriwa na mgombea mwenza wa chama hicho Dk. Emmanuel Nchimbi.
