Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia, Dodoma

Serikali imetaja sekta tano zilizoongoza kwa kasi ya ukuaji wa uchumi nchini mwaka 2024 kuwa ni sanaa na burudani, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme, habari na mawasiliano, pamoja na fedha na bima na afya.

Akizungumza bungeni wakati akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/26, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema sekta ya sanaa na burudani ilikua kwa kasi zaidi kwa asilimia 17.1.

Amesema sekta nyingine zilizoshuhudia ongezeko kubwa ni uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme (14.4%), habari na mawasiliano (14.3%), fedha na bima (13.8%) na afya (10.1%).

“Tunahitaji kuongeza tija zaidi katika iuzalishaji ili kilimo kiweze kuinua kipato cha Watanzania walio wengi zaidi,” alisema Prof. Mkumbo.