Mchezaji wa zamani wa Real Madrid, Sergio Ramos, ameingia rasmi kwenye muziki kwa kuachia wimbo wake wa kwanza wa solo uitwao “Cibeles”, uliozinduliwa Agosti 31, 2025.
Wimbo huu unaelezea kumbukumbu zake na upendo kwa Real Madrid, klabu aliyotumikia kwa miaka mingi. Ramos anagusia pia maumivu ya kuondoka Bernabéu bila kutaka, akisema: “Sikuwahi kutaka kuondoka, wewe ndiye uliyeomba niruke.”
Hapo awali Ramos alishiriki kwenye nyimbo kama “La Roja Baila” na “Otra estrella en tu corazón”, lakini “Cibeles” ndiyo wimbo wake wa kwanza akiwa msanii huru.
Kutoka uwanjani hadi studio, Ramos anaonesha kuwa safari yake ya sanaa bado inaendelea. Je, ataendelea kufanikiwa kwenye muziki kama alivyo kwenye soka?
