Serikali itaendelea kuhakikisha nguvu kazi ya Taifa inakuwa na ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira ili kuongeza tija kazini na ushindani wa uzalishaji.
Hatua hiyo inalenga kujenga nguvu kazi yenye ujuzi, maarifa na weledi unaokidhi mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya soko la ajira la sasa na baadaye.
Hayo yamebainishwa leo Januari 13, 2026 Jijini Mbeya na Mkurugenzi Msaidizi wa Ukuzaji Ajira, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Godwin Mpelumbe, wakati wa Mafunzo ya ukuzaji ujuzi kwa wakulima wa zao la Maharage.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima waliohudhuria mafunzo hayo akiwemo Rehema Mchiwa, wamesema elimu waliyoipta itaongeza uzalishaji, kuboresha ubora wa mazao na kuinua thamani ya zao la maharage.






