Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma

Serikali imesema kumekuwa na ongezeko la hali ya unene na unene uliokithiri.

Kauli hiyo imetolewa bungeni mjini Dodoma leo na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama alipokuwa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026.

“Takwimu zinaonesha ongezeko la hali ya ufanyaji mazoezi, hata hivyo kumekuwa na ongezeko la hali ya unene na unene uliokithiri kutoka asilimia 26.0 mwaka 2012 hadi asilimia 30.8 mwaka 2023.

“Vilevile, kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) idadi ya wagonjwa wapya wa saratani imeongezeka kutoka visa vipya 40,464 na vifo vitokanavyo na saratani 26,945 mwaka 2020 na kufikia visa vipya 44,931 na vifo 29,743 mwaka 2022 mtawalia. “ amesema Waziri Mhagama.