Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Serikali imeongeza muda wa kujisali baada ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DAR – PC) kuiomba Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari nchini kuongeza muda wa usajili wa waandishi wa habari kwa siku 10 zaidi, ili kutoa fursa kwa waandishi wengi zaidi kutimiza takwa hilo la kisheria.
Ombi hilo limetolewa leo Juni 21, 2025 jijini Darces Salaam na Mwenyekiti wa DAR PC, Bakari Kimwanga, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kimwanga, muda uliotolewa kwa sasa umemalizika leo, Juni 21, 2025, hali inayowatia changamoto baadhi ya waandishi ambao bado hawajakamilisha mchakato wa usajili.
Amesema usajili wa waandishi wa habari si tu ni suala la kutimiza matakwa ya kisheria, bali pia ni hatua muhimu ya kuthibitisha weledi na uwajibikaji wa taaluma ya uandishi wa habari nchini.
Mkutano huo Mkuu wa DPC umewakutanisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu mustakabali wa taaluma hiyo, ikiwa ni pamoja na maadili, haki za waandishi, na maendeleo ya kitaaluma ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mwanzo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo.

Kutokana na ombi hilo Serikali imeongeza muda wa kujisajili hadi Juni 28, 2025 ili kutoa muda kwa waandishi wa habari ambao bado na waliopata changamoto wakati wa usajili.





