π Dkt. Biteko amwakilisha Makamu
wa Rais, Dkt Philip Mpango maadhimisho ya miaka 125 Parokia ya Kome – Geita
π Rais Samia achangia Tsh.Milioni 50 Ujenzi wa mradi wa maji Parokia ya Kome
π Maaskofu Waishukuru Serikali kwa ushirikiano na Taasisi za dini
Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali itaendelea kuziunga mkono na kushirikiana na taasisi zote za dini ili kuleta na kuchagiza maendeleo na Ustawi wa wananchi.
Dkt. Biteko amesema hayo Agosti 17, 2025 wakati akimwakilisha Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango kuwa mgeni maalum katika maadhimisho ya miaka 125 ya Ukristo na Uinjilishaji katika Parokia ya Kome, Jimbo Katoliki la Geita.

β Niseme Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zote za dini katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hii ni kuhakikisha wananchi wanapata maendeleoβ amesema Dkt. Biteko na kuongeza kuwa Serikali inafarijika kuyokana na mchango wa taasisi za dini kuwaletea wananchi maendeleo katika maeneo yao.
Sambamba na ibada hiyo ya Jubilei, Dkt. Biteko ameongoza Changizo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kwa ajili ya huduma katika makazi ya Masisita, Parokia ya Kome.
Akizungumza mara baada ya misa, Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhasham FLavian Kassala Maombi ya Baraka kwa mchakato wa kupata viongozi na mchakato wa kupata viongozi sahihi katika uchaguzi Mkuu ujao mwezi Oktoba, 2025.

Mhasham Askofu Kassala ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya awamu ya sita kufuatia ushirikiano wa Serikali kwa taasisi za dini ambazo zimekuwa chachu ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini
Amesema huduma ya maji safi na salama katika Kisiwa cha Kome bado ni changamoto hivyo, ameiomba Serikali kufanikisha mpango wa upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa Kome.
β Pamoja na kwamba hapa ni kisiwa na tumezungukwa na maji, huduma ya maji safi bado ni ndogo na wananchi wenye uwezo wa kupata maji ni wachache,β amesema Askofu Kassala
Amesema Kanisa liko katika jitihada za kusogeza huduma za jamii kwa kuongeza watawa zaidi ambo watatoa huduma za jamii na hiyo wanahitaji huduma za haraka.

Dkt. Biteko amesema serikali itafanya upembuzi ili kuhakikisha huduma hiyo ya maji ili kuhakikisha watawa wanapata maji.
Amewaomba wakazi wa Kome kuzidisha moyo wa ushirikiano sambamba na kuboresha mazingira na kupanda miti ili kulinda na kurejeaha uoto wa asili.
Aidha, amechangia kiasi cha shilingi milioni 10 huku akiwasilisha mchango wa shilingili milioni 50 kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya kufanikisha azma ya kufanikisha upatikanaji wa huduma ya maji katika makazi ya watawa Kome.
Awali akihubiri katika ibada ya maadhimisho ya miaka 125 tangu kuanzishwa kwa utume katika Parokia ya Kome, Askofu Mkuu wa Jumbo Kuu la Mbeya, Mhasham Gervas Nyaisonga amewataka waumini kushikamana, kuvumoliana na kujenga maelewano katika jamii.

β Tunapoadhimisha miaka 125 ya utume tunitahidi kuelewq kuwa tunatakiwa kustawisha umoja na utulivu miongoni mwetu, sisi ni wadhaifu tuna mapungufu tumgeukie Mungu na kuomba nguvu.β anesema Askofu Mkuu Nyaisonga.
Akizungumzia uchaguzi Mkuu ujao, Nyaisonga amewataka wakatoliki kufanya maombi maalum kwa saa 24 kuanzia Agosti 23-24 mwaka huu ili kufanikisha uchaguzi wa amani utakaowezesha upatikanaji wa viongozi bora.




