Na Rahma Khamis, Zanzibar

NAIBU Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Mhe Hassan Khamis Hafidh amesema Serikali ya Awamu ya nane ipo tayari kushirikiana na vyama vya ushirika ili kuwainua kiuchumi

Aliyasema hayo katika Ukumbi wa Umoja wa Washirika wa Uchukuzi Bandarini Wilaya ya Mjini katika ziara kutembela Taasisi zilizomo katika Wizara yake na kujitambulisha

Alisema kuwa vyama vya Ushirika vina Mchango mkubwa katika kukuza Uchumi hivyo Serikali itaunga mkono juhudi zinazofanywa na vyama hivyo ili kufikia lengo lililokusudiwa

Alisema kuwa Kuwepo wa vyama hivyo kunasaidia kujikomboa kiuchumi na kuinua kipato Cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla

Naibu Waziri alifahamisha kuwa Serikali ina jukumu la kuhakikisha vyama vya ushirika vinafanya kazi kwa kufuata taratibu ili kuondoa umasikini.