Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,
Dar es Salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imejidhatiti kuhakikisha inafanya mageuzi makubwa ya elimu ujuzi kwa vitendo kuhakikisha wanaongeza vyuo vya Veta ili kusaidia vijana wanapata ujuzi katika fani mbalimbali ili wasitegemee kuajiriwa bali wajiajiri na kukuza uchumi wa nchi.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amebainisha Serikali ya Awamu ya Sita imejiwekea mipango mikakati madhubuti inayokwenda na mwelekeo mpya kuibadilisha kwa kasi sura ya fursa kwa vijana, huku kipaumbele kikisogea zaidi kwenye maandalizi ya nguvu kazi katika elimu ya amali katika teknolojia na ubunifu wa kisasa.

” Bajeti ya Wizara ya elimu imeongezeka kwa asilimia 40 na imekuwa chachu ya kujenga Mradi ya vyuo vya Veta katika mikoa mtano kutekeleza ws kampasi ya chuo kikuu kila mkoa shule za ufundi hii inakwenda kuweka twaswira chanya kwa Vijana watakaojiajiri ” amesema Waziri.
Sanjari na hayo Waziri wa Elimu amebainisha kuwa Serikali imekuwa ikitoa chachu kwa Wanafunzi wanafanya vizuri katika ufaulu mzuri katika masoko ya Sayansi kupitia mpango wa Samia Scholarship, kuwapeleka katika masoko nje nchi na tayari wanaanza kundi la kwanza la wanufaika 50 linatarajiwa kwenda Afrika Kusini kusomea Artificial Intelligence na Data Science.
Haya si mageuzi ya leo kwa kesho; ni uwekezaji wa vizazi vyetu. Ndiyo maana tunasema elimu sasa ni injini ya mabadiliko ya taifa.” amesisitiza Prof Mkenda
Sambamba na hayo uwezeshaji mwingine, Waziri amesema, “Kupitia COSTECH na CRDB imetengwa shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya vijana wabunifu kwa kuleta bunifu zao zinazoleta suluhisho za Changamoto zinazoikabili Jamii na kuleta matokeo, si ndoto tu.”

Katika upande wa elimu ya ufundi, serikali imekuwa ikijenga vituo vya VETA katika kila wilaya. Prof. Mkenda alisema ada nafuu ya shilingi 60,000 kwa wanafunzi wa kutwa na shilingi 120,000 kwa wanaoishi hosteli imewekwa ili
Serikali imeamua kusaidia vijana wapate ujuzi kwa gharama nafuu Tsh 120,000 kwa wanaoishi hosteli imewekwa ili kufungua milango ya ujuzi hata kwa familia zenye kipato cha chini zinufaike kwani mabadiliko hayo yameanza kubadili mtazamo wa jamii kuhusu mafunzo ya ufundi, ambayo awali yalionekana kama chaguo la mwisho.
Kuhusu ubunifu, Waziri amefafanua Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi bunifu, akisema, ambapo Mahindi wa Kwanza huzawadiwa Milioni 10 na KAZI yake inanuliliwa hii inaleta chachu kwa jamii izoe kufikiri na kubuni.



