Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba, ametangaza leo bungeni kuwa Serikali imeyafutia Kodi ya VAT magazeti yote yanayozalishwa nchini.

Hatua hii itatoa ahueni kubwa kwani kati ya chanzo cha kifo cha magazeti imekuwa hii Kodi ya VAT.

Imekuwa kila mara unatoa risiti ya EFD kwa matangazo, alafu hiyo risiti inachelewa kulipwa tunadaiwa VAT ambayo hatujapokea.

Kwa maana hiyo, magazeti sasa katika matangazo yatakua hayatozi VAT nayo hayadaiwi VAT.

Kutokana na umuzi huo mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema kuwa hiyo ni hatua kubwa na ya ukombozi kwa magazeti aliyoifanya Rais Samia Suluhu Hassan.