Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar
Serikali imesema sekta ya uchukuzi ,imeendelea kukua kwa kuongeza pato
la taifa kutoka asilimia 7.1 hadi 7.5 kwa mwaka 2024.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa kuhusu utendaji wa serikali katika siku 100 za uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere.
Msingwa amesema mkutano huo. ni mwendelezo wa mikutano ambayo amekuwa
akiifanya katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuelezea utekelezaji wa shughuli na miradi ya Serikali kwenye maeneo yanakotekelezwa miradi ili wananchi wapate fursa ya kusikia na kujionea maendeleo hayo.

“Nimeamua kuufanyia mkutano huu katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa makusudi, ili kuwaonesha Watanzania kazi kubwa iliyofanywa na serikali katika kuimarisha sekta ya uchukuzi.
Msingwa amesema .katika sekta hiyo ,Serikali imefanikiwa katika uendelezaji wa viwanja vya ndege nchini kupitia Mamlaka yaViwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Pia kwenye huduma za usafiri wa anga kupitia Kampuni ya Ndege Tanzaniana uUtekelezaji wa miradi na uendeshaji wa reli, ikiwemo ununuzi wa mabehewa na ufanisi katika kuhudumia abiria na mizigo.
‘’Uendelezaji wa bandari na usafiri majini,usalama wa usafiri majini na huduma za uokoaji na maendeleo ya sekta ya utalii” amesema.

Msigwa amesema maeneo hayo,ni mhimili muhimu kwa uchumi na yana mchango mkubwa katika kukuza biashara, uwekezaji utalii na ajira kwa Watanzania.
Amesema serikali imefanya uendelezaji wa viwanja vya ndege na usafiri wa anga,katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/25 na nusu ya mwaka 2025/2026
‘’Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imeendelea kuwekeza kwa kiwango
kikubwa, katika uboreshaji na upanuzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege nchini kwa lengo la kuongeza ufanisi, usalama na ubora wa huduma za anga’ ’amesema.
Aidha amedai Serikali imeendelea ,kuimarisha usalama katika maeneo ya viwanja vya ndege, kwa kununua mashine za kisasa 13 za ukaguzi wa abiria na mizigo na kuzifunga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Uwanja wa Kigoma, Shinyanga, Tanga, Lake anyara na
Iringa.
Ambapo hatua hizi zimeongeza ubora wa huduma na kuruhusu viwanja husika kutoa huduma mchana na usiku.

Aidha amesema miradi yakimkakati ,inayoendelea kutekelezwa Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2022/23 hadi 2024/2025 Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika viwanja vya ndege yenye thamani ya shilingi trilioni 1.154.
Inayolenga kuongeza uwezo wa Viwanja vya Ndege ,katika kuhudumia
ndege, abiria na mizigo na kuboresha usalama, ulinzi na uwezeshaji katika Viwanja hivyo.
Msingwa amesema baadhi ya miradi iliyotekelezwa katika kipindi hicho, imekamilika kwa asilimia 100 na mingine ipo hatua za mwisho.



