Na Jovina Massano
WAZALISHAJI wa bidhaa za vilipuzi inazotumika migodoni waiomba serikali kuwapa kipaumbele wa soko ili kuwawezesha kuongeza wigo mpana wa kuongeza nafasi za ajira hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Mhandisi Joseph Richard Juma kutoka SOLAR NITROCHEMICAL LTD watengenezaji wa vilipuzi kutokea mkoani Pwani -Kisarawe wakati wa hitimisho la kongamano la maonyesho ya madini katika viwanja vya shule ya msingi Mukendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Joseph ameishukuru Wizara ya Madini na ofisi ya madini pamoja na mkuu wa mkoa wa Mara kwa kuweza kuwakutanisha na wadau mbalimbali wakiwemo wachimbaji wakubwa,wa kati na wadogo moja kwa moja.
” Tunaiomba serikali itupatie kipaumbele kwa kutupa nafasi ya kusambaza bidhaa zetu nchi nzima hasa maeneo yenye migodi Kama walivyoweka sheria ya raia wageni kupewa leseni za wachimbaji wadogo kwa kiasi kikubwa wenye migodi huagiza vilipuzi nje ya nchi “, amesema Joseph.
Ameongeza kuwa Kampuni hiyo huzalisha vilipuzi vya aina zote vinavyotumika migodini kwa wachimbaji wakubwa ,wa kati na wadogo.
Nae mchimbaji mdogo Jackson Nyamachoa kutoka mgodi wa Irasanilo uliopo Kata ya Mirwa Kijiji Cha Magunga wilayani Butiama amesema kuna haja ya serikali kuwapa vipaumbele wazalishaji wa ndani kwa kuwa wanainua uchumi wa nchi kwani kutasaidia vijana kupata ajira na wasambazaji na wauzaji kupata unafuu kwa kufuata karibu.

“Naiomba serikali itengeneze mfumo ambao utawezesha upatika wa bidhaa kwa wakati kwa kuwa wazalishaji hao ni walipa kodi za serikali na kuna muda bidhaa hizo wanaozileta kutoka nje ya nchi huchelewesha na huadimika vilevile,”amesema Jackson.
Amewaomba watengenezaji wa vilipuzi waliopo nchini kutembelea katika migodi ilikuweza kuongeza wigo wa biashara hiyo na washirikiane na ofisi za madini kwenye maeneo yenye migodi.




