Serikali yapendekeza kukusanya na kutumia trilioni 62.334/- kwa mwaka wa fedha 2026/27
JamhuriComments Off on Serikali yapendekeza kukusanya na kutumia trilioni 62.334/- kwa mwaka wa fedha 2026/27
Na. Peter Haule na Josephine Majura, WF, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, (Mb), amewasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27, ambapo katika kipindi hicho, inatarajia kukusanya nakutumia shilingi trilioni 62.334 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, maendeleo na kulipia deni la Taifa.
Mhe. Balozi Omar amesema hayo wakati akiwasilisha Mpango huo ambapo amesema kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 10.3 ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha, 2025/26.
Tukio hilo limeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na kuhudhuriwa pia na Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu, na viongozi waandamizi wa Serikali.
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, (Mb), akiwasilisha bungeni jijini Dodoma, Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2026/2027 kwenye Kamati ya Bunge zima, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 62.334. kwa mwaka 2026/27, sawa na ongezeko la asilimia 10.3.Mawaziri, Wabunge na Viongozi wengine wakiwa katika Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Mbungeni jijini Dodoma ambapo yamewasilishwa Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2026/2027.Naibu Waziri wa Fedha, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akifuatilia jambo kabla ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2026/2027 kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Mbungeni jijini Dodoma.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azan Zungu, akitetea jambo na Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, (Mb) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu,Mhe. William Vangimembe Luvuki, baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2026/2027 kwenye Kamati ya Bunge zima, bungeni jijini Dodoma.