Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza zaidi ya bilioni 17.8 kutoka bilionin13.6 katika ununuzi wa mitambo ya uchunguzi ili kutoa huduma bora za uchunguzi wa Kisayansi wa kimaabara kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa leo Julai 10, 2025 na Mkurugenzi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (MMS), Dkt. Fidelice Mafumiko wakati akiwasilisha mada kwa wahariri wa vyombo vya habari katika kikaokazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.

“Uwekezaji katika ununuzi wa mitambo ya uchunguzi wa kimaabara umeongezeka kwa
asilimia 23.6, kutoka Shilingi Bilioni 13.6 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi
2021/2022 hadi kufikia thamani ya jumla ya Shilingi Bilioni 17.8 kwa mwaka wa Fedha
2024/2025 kwa kuongeza mitambo mikubwa Kumi na Sita (16) na midogo 274.
” Ununuzi wa mitambo hii umeendelea kuimarisha uchunguzi wa kimaabara nankuendelea kutoa huduma bora za uchunguzi wa Kisayansi wa kimaabara kwa wananchi kwa ufanisi zaidi” alisema Dk Mafumiko.
Amesema kuwa ubora wa huduma zinazotolewa na MMS, Dkt. Mafumiko alisema kuwa mamlaka imefanikiwa kutoa huduma za uchunguzi wa kimaabara zinazokubalika kitaifa na kimataifa kwa kutekeleza mifumo ya ubora na umahiri yenye viwango vya kimataifa kama ISO 9001:2015 na ISO 17025:2027.
Amebainisha kuwa katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita, MMS imefanikiwa kupata ithibati ya mfumo wa umahiri wa uchunguzi wa kimaabara (ISO 17025:2027) katika maabara sita ambazo ni: Maabara ya Vinasaba vya Binadamu, Mikrobiolojia, Sayansi Jinai, Toksikolojia, Mazingira, Maabara ya Chakula na Kanda ya Ziwa – Mwanza.

“Mafanikio haya ni makubwa na muhimu kwa kuwa, kunaifanya Mamlaka kukidhi matakwa
ya Kisheria na mifumo ya Ubora katika ngazi ya kitaifa na kimataifa” alisema.
Mkurugenzi aliongeza kuwa Mamlaka inatekeleza jukumu la usimamizi na udhibiti wa kemikali kupitia utekelezaji wa
Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani, Sheria Na. 3.
ya Mwaka 2003.
“Lengo la Sheria hii ni kulinda afya na mazingira dhidi ya madhara ya
kemikali.
“Aidha, utekelezaji wa sheria hii unafanyika kupitia usajili wa wadau, ukaguzi wa maghala na maeneo ambapo kemikali zinatumika, ukaguzi wa maeneo ya mipaka ambapo
mizigo yote ikiwemo kemikali zinapitia, na utoaji vibali vya kuingiza au kusafirisha kemikali ndani na nje ya nchi” amesema.

Amesema kuwa mamlaka imeendelea kufanya maboresho ya kuharakisha mchakato wa usajili wa kampuni zinazojihusisha na biashara ya kemikali.
“Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita kumekuwa na ukuaji wa biashara kwa wadau wanaojihusisha
na biashara ya kemikali.
” Wadau waliosajiliwa wameongezeka kutoka Wadau 2,125 Mwaka 2021 hadi Wadau 3835 kufikia Juni, 2025 sawa na ongezeko la asilimia 81 la wadau waliosajiliwa” amesema.

Aliongezsla kuwa katika kuhakikisha kuwa kemikali zinatumika kwa usalama na kwa kufuata taratibu zote
zinazohitajika ili kulinda afya ya binadamu na mazingira, na pia ili kuhakikisha kuwa
kemikali zinazoingizwa nchini ni zile ambazo zinaruhusiwa kisheria kuingia nchini.
“Mamlaka hufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye maghala yanayohifadhi kemikali na maeneo ya mipaka. Hivyo, katika kipindi cha miaka minne (4) cha Serikali ya awamu
ya sita (6), Mamlaka imefanya ukaguzi wa maghala 8,521 ya kuhifadhia kemikali sawa
na asilimia 119 ya lengo la kukagua maghala 7,160.
Dk Mamlaka imeweza kudhibiti uingizaji na usafirishaji wa kemikali hatarishi na zile
zinazodhibitiwa chini ya mikataba ya kimataifa ili kulinda afya ya binadamu, mazingira na usalama wa nchi kwa kutoa vibali vya kuingiza na kusafirisha kemikali hizo.

Katika kipindi cha miaka minne (4) cha Serikali ya awamu ya sita (6), kumekuwa na ongezeko la vibali vya uingizaji wa kemikali kutoka vibali 40,270 kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 hadi vibali 67,200 kufikia kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 40 ya vibali vilivyotolewa.
Ongezeko hili la vibali limetokana na kuwepo kwa mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji yaliyowekwa na Serikali ya awamu ya sita, wadau kuongeza uelewa wa Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali inayosimamia shughuli za kemikali kwa kujengea uelewa wa matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA inayotumika katika uombaji wa usajili na vibali.





