Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia,
Dar es Salaam

Mgombea wa Jimbo Jipya la Chamanzi kwa Tiketi ya Chama cha Wakulima AAFP Shani Kitumbua amewaomba Wananchi ridhaa ya kumchagua nafasi aliyoimba kwani atakwenda kutatua kero ikiwemo kuisemea barabara ya Kilungule ambayo ni Mbovu,uchache wa Shule na matukio ya kihalifu yanayotishia raia

Hayo amebainisha Leo Agosti 19,2025 akizungumza na Waandishi wa habari Temeke Dar es salaam mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo hilo kutoka kwa Msimamizi Mkuu Uchaguzi Temeke Fortunata Shija amesema Chamanzi palisahaulika kimaendeleo Shule ni chache wanafunzi ni wengi hivyo akipewa Dhamana atakwenda kuleta suluhu.

” Mimi kama nitakuwa Mbunge nitakwenda kuhakikisha wanafunzi wanasoma vizuri kwa kuondoa fedha wanazoagizwa kila siku na waalimu siku za mapumziko wakisingizia ni masomo ziada”Amesema Shani.

Sambamba na hayo amebainisha kuwa barabara ya Kilungule imekuwa sumbufu muda mrefu trafiki wameifanya ya kupigia hela kutoka kwa madereva daladala bajaji na Pikipikia.