Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, ametaja mafanikio makubwa ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameyafanya ndani ya siku 100 madarakani ikiwemo kuwawezesha vijana.

Akizungumzia siku 100 za Rais Samia IKULU, Waziri Nanauka, Waziri Nanauka alisema Rais Samia amefanikiwa kutekeleza ahadi zake hasa kusaidia vijana wa makundi mbalimbali ambao wengi wamepata mafunzo ya ujasiriamali na kupata mikopo.

Akizungumzia siku 100 za Rais Samia IKULU, Waziri Nanauka, alisema kwa utekelezaji wa ahadi zake ndani ya siku 100 IKULU, Rais Samia amevunja rekodi ya watangulizi wake.

“Siku 100 za Rais Samia IKULU zimekuwa na mafanikio makubwa sana na pengine naweza kusema ni kati ya siku 100 zenye matokeo ya haraka kuliko na hii inatokana na dhamira yake,, aliahidi bilioni 200 kwa wafanyabishara wadogo, wakati na wa kampuni changa na amezitoa,” alisema

Waziri Nanauka alisema kati ya ahadi 13 alizotoa Rais Samia kuwa atazitekeleza ndani ya siku 100, ahadi sita zinahusu maendeleo ya vijana ambazo ni asilimia 46 ya ahadi hizo.

“Kwa maana nyingine katika siku zile 100 tungekuwa tunazigawa, siku 46 alikuwa anashughulika na vijana na mabadiliko mengi yameonekana kwa vijana kupata mafunzo ya ujuzi, mitaji midogo midogo imewafikia vijana wanaokuza biashara zao,” alisema.

Alisema mambo mengi yamefanyika ndani ya siku 100 za Rais Samia ikiwemo kuanzishwa kwa vituo vya teknolojia ya ubunifu na kufungua milango ya dunia kidijitali kwa vijana.

“Wizara imechagua kusikiliza mawazo ya vijana, na mawazo yao yamesikika na yamekuwa dira na mipango na maamuzi na maelfu ya vijana wamepata mafunzo, mamia wamwezeshwa kifedha na program mpya za michezo zimeanzishwa,” alisema

“Kila kijana wa nchi hii anayonafasi sawa kama atajitambua ataamua kufanya anachokitaka na kuwekeza kwenye kile anachotaka kufanya, kila kijana ndani yake kuna kitu,” alisema Waziri Nanauka

Mmoja wa vijana aliyepata mafunzo na mtaji ndani ya siku 100 za Rais Samia, aliwataka vijana kufanyakazi kwa bidii kwani mafanikio humfuata kijana anayejituma.

“Vijana wafanye kazi, mimi nimepata mafunzo nimeanzisha biashara inakwenda vizuri kwa hiyo nawaasa vijana wasidhani kwamba mafanikio yanakuja kwa bahati, lazima wafanye kazi kwa bidii,” alisema.

Mjasiriamali mwingine, Andrew Siza, alisema ndani ya siku 100 vijana wengi wamefanikiwa kupata mafunzo ya ujasiriamali na wengi wamepata mtaji wa kuanzisha biashara.

Vijana wa Bukoba na Mwanza wanaojihusisha na ufugaji kwenye vizimba nao wamenufaika na siku 100 za Rais Samia IKULU kwa kupata mafunzo ya biashara na ujasiriamali pamoja na mikopo midogo.

Gasper Urio ambaye ni mmoja wa vijana wanaofuga samaki kwenye vizimba Mwanza alimshukuru Rais Samia kwa kuendelea kutekeleza ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

“Tunamshukuru Rais Samia kwa kutekeleza ahadi zake, kama ameweza kufanya mambo haya makubwa ndani ya siku 100 tunaamini mbele kuna mwanga zaidi na atafanya makubwa zaidi kwa vijana, sisi wafuga samaki tumenufaika sana na mafunzo ya biashara,” alisema