Simba SC kwenye nafasi nzuri kuelekea mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki ijayo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Nsingizini FC ya Eswatini

Ushindi wa jumla wa michezo hiyo miwili atasonga mbele kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Nsingizini FC ya Eswatini, katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya pili ya michuano hiyo, uliochezwa leo Oktoba 19, 2025.

Mabao ya Simba yalifungwa na Wilson Nnang’u dakika ya 45+2 kipindi cha kwanza, kabla ya Kibu Denis kuhitimisha ushindi huo kwa mabao mawili dakika ya 85 na 90+1.