Watani wa jadi Simba SC na Yanga SC wamefanikiwa kutoka sare tasa ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo, Machi 1, 2026, katika Uwanja wa Amani, Visiwani Zanzibar.
Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa, huku Simba SC wakionekana kuwa bora katika kipindi chote cha mchezo.
Yanga SC wanafikisha pointi 29 wakiwa katika nafasi ya kwanza, huku Simba SC wakifikisha pointi 24 katika nafasi ya tatu. Huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 11 kila moja.


