Na Mwandishi Wetu,Jamhuri Media
Dar es Salaam

Katika kuunga Mkono Jamii suala la Afya Taasisi ya Rivaivu(Revive) iliopo jijini Dar s Salaam jirani na Hospitali ya Ocean Road inatarajia kuadhimisha siku ya kimataifa ya matibabu ya Physiotherapy kutoa huduma za matibabu ya hayo bila malipo Septemba 6 hadi 7 hivyo wananchi wanashauriwa kujitokeza kupata huduma hiyo bure

Akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji na Muasisi wa Taasisi hiyo ya Revive Dk Lekhani Pashine amesema wameamua kuadhimisha siku hiyo kwa kutoa huduma za matibabu ya Physiotherapy ili kuongeza uelewa wa tiba hiyo kwa jamii.

Mmoja wa wataalamu wa tiba hiyo Nathanaeli Stanley akifafanua kuhusu huduma hiyo na amewashauri wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma bure bila malipo.

Hata hivyo mtaalamu huyo wa matibabu ya Physiotherapy Nathanael Stanley ametumia mchoro wa uti wa mgongo wa binadamu kueleza maradhi ya maumivu ya viungo na tatizo la ganzi miguuni linavyotokea na matibabu hayo yalivyo.

Naye Mtaalamu wa Physiotherapy kwa watoto ,Dianarose Mtery amewashauri wazazi wenye watoto wenye utindio kujitokeza kwa wingi

Maadhimisho ya siku ya Physiotherapy Unitarian kimataifa kila mwaka hufanyika Septemba 8 lakini hospitali ya Revive wameamua kufanya maadhimisho hayo siku za mwisho wa wiki ili kuhudumia watu wakiwa mapumziko ambapo huduma zitafanyika kwenye kituo kilichopo Posta jirani na Hospitali ya Ocean.