Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar ea Salaam

Shamrashamra za ufunguzi wa Tamashara la Sauti za Busara linalojulikana kama Tamasha rafiki zaidi Dunia ,zimeendelea kushika kasi na maandalizi yapo katika hatua za mwisho.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari ,Mkurugenzi mkuu wa Tamasha Promotions Lorenz Herrmann amesema Tamasha litafanyika kuanzia Alhamisi Februari 5 hadi 8, 2026.

Ambapo likiwa na ufunguzi wa awali (soft opening) Jumatano tarehe 4 Februari, katika makazi mapya Viwanja vya Mnazi Mmoja, Stone Town.

Amesema Busara Promotions imethibitisha kuwa hatua hiyo, imewezesha kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kupokea hadhira, kuboresha mtiririko wa watazamaji, na kuinua uzoefu wa wasanii na mashabiki kwa ujumla.

Amesema kwa zaidi ya miaka 22, Ngome Kongwe (Old Fort) imekuwa kitovu cha kihistoria na alama ya tamasha hivyo hatua ya kuhamia Viwanja vya Mnazi Mmoja kunaashiria hatua muhimu ya mabadiliko

‘’Kwani eneo jipya linatoa nafasi pana, mandhari ya kijani na upepo wa bahari pamoja na faida za kiutendaji kama usalama na urahisi wa ufikaji.

Kwa upande wa kiuchumi, Tamasha linawezesha wafanyabiashara wengi
zaidi, hadhira kubwa , programu pana zaidi na kitamaduni linaonesha mwendelezo bila kusimama,amesema.

Amesema Tamasha linakua, lakini misingi na maadili yake yanaendelea kubaki imara zaidi ya majukwaa makuu, programu shirikishi za pembeni za Sauti za Busara zinaendelea kuongeza mvuto wake.

‘’Matembezi ya Carnival parade huyageuza Stone Town kuwa jukwaa linalotembea, likivunja mipaka kati ya msanii na mtazamaji.

Swahili Encounters huwakutanisha wanamuziki kutoka nchi mbalimbali ili
kufanya mazoezi na kuwasilisha maonesho ya pamoja, yakitoa kipaumbele kwa mchakato wa ubunifu kuliko onesho pekee.

Majukwaa ya kitaaluma kama Movers & Shakers hutoa nafasi muhimu ya mijadala ya kitaaluma-nguzo inayopuuzwa mara nyingi katika uendelevu wa uchumi wa ubunifu” amesema.

Amesema Tamasha pia linafika nje ya Stone Town kupitia Busara Plus, jukwaa la bure la kijamii linalofanyika katika maeneo kama Fumba Town Nyamanzi.

Amesema utamaduni unapaswa kusambaa, si kujikusanya mahali pamoja kwa
vijana na wasanii wanaoanza

Hutoa fursa ya kuonekana bila vikwazo vya kifedha- gharama ndogo kiuchumi, lakini muhimu sana kitamaduni ushirikishwaji wa kijinsia unaendelea kupewa uzito mkubwa.

Wanawake wanaonekana si tu kama wasanii, bali pia waandaaji, wasimamizi, wazalishaji na mafundi wa kiufundi katika tasnia ambayo
mara nyingi mchango wa wanawake hautambuliwi ipasavyo,

Amedai Sauti za Busara inaonesha kwa vitendo viwango vipya ambapo uonekano unakuwa sera, na uwakilishi unakuwa vitendo.

Viwanja vya Mnazi Mmoja vitakuwa na majukwaa kadhaa ya muziki, maeneo
ya wazi yenye kivuli chini ya miti ya asili ijulikanayo kama Mivinje na Mikaratusi.

Aidha soko la chakula na bidhaa za mikono, maeneo ya mitandao ya kitaaluma, pamoja na urahisi zaidi wa kufikika kwa watembea kwa miguu, usafiri wa umma na magari binafsi.

‘’Mahitaji ya toleo la 2026 yamefikia viwango vya juu zaidi kuwahi kushuhudiwa kwani tiketi za Awali (early Bird) kuuzwa zote, huku
tiketi za Mapema(Advance) zikiendelea kuuzwa kwa kasi

Hii inachangiwa na orodha ya wasanii wa kiwango cha dunia, ikiwajumuisha zaidi ya wanamuziki 400 kutoka nchi 21 barani Afrika na duniani kote.

Kinara wa tamasha ni gwiji wa muziki kutoka Mali, Salif Keita, ambaye urithi wake wa muda mrefu na wimbo wake uliosambaa kimataifa “Yamore” umevutia mashabiki wa muda mrefu pamoja na kizazi kipya duniani’’amesema.

Journey Ramadhan, Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara.amesema mwitikio wa mwaka huu umekuwa wa kipekee sana,

Kwani mchanganyiko wa eneo jipya kubwa, orodha bora ya wasanii inayoongozwa na Salif Keita, pamoja na ongezeko la hamasa ya
kimataifa, umeifanya kuwa moja ya matoleo yanayosubiriwa kwa hamu zaidi katika historia .

Ramadhani amesema ushirikiano wao wa karibu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mamlaka husika umetuwezesha kupanua tamasha kwa usalama ili kukidhi mahitaji .

” Zaidi ya muziki, Sauti za Busara 2026 inaendelea kujitofautisha kupitia mchango wake mkubwa wa kijamii na kitamaduni.

Aidha uanzishaji wa kwanza wa programu ya ‘Inspire to Lead!’ulifanyika kwa mafanikio makubwa tarehe 17 Januari 2026 katika Viwanja vya Kibanda Maiti, ukivutia ushiriki mpana na mwitikio chanya.

Uanzishaji huu ni sehemu ya Mpango wa Mabadiliko ya Kijinsia (Gender
Transformative Action Programme) unaolenga kutokomeza ukatili dhidi ya
wanawake na wasichana,

Kuendeleza uongozi wa wanawake, na kuhamasisha kampeni kama Tokomeza
Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na Rijali Anajali’’. amesema

Ofisa Programu wa Busara promotions ,Zakialulu Mdemu amesema Jukwaa
lao linawawezesha kuwafikia maelfu ya watu kupitia utamaduni.

Mdemu amesema kuunganisha programu ndani ya uzoefu wa tamasha, wameongeza uelewa kuhusu Vituo vya Huduma za Jinsia (One-Stop Gender Centres) na huduma muhimu zinazotolewa na Serikali ya Zanzibar, huku wakisherehekea uongozi, ustahimilivu na usawa